Date: 
17-08-2017
Reading: 
Hebrews 12:7-13 NIV (Waebrania 12:7-13)

THURSDAY   17TH   AUGUST   2017   MORNING                               

Hebrews 12:7-13 New International Version (NIV)

Endure hardship as discipline; God is treating you as his children. For what children are not disciplined by their father? If you are not disciplined—and everyone undergoes discipline—then you are not legitimate, not true sons and daughters at all. Moreover, we have all had human fathers who disciplined us and we respected them for it. How much more should we submit to the Father of spirits and live! 10 They disciplined us for a little while as they thought best; but God disciplines us for our good, in order that we may share in his holiness. 11 No discipline seems pleasant at the time, but painful. Later on, however, it produces a harvest of righteousness and peace for those who have been trained by it.

12 Therefore, strengthen your feeble arms and weak knees. 13 “Make level paths for your feet,”[a] so that the lame may not be disabled, but rather healed.

Footnotes:

  1. Hebrews 12:13 Prov. 4:26

God loves us and because he loves us He must discipline us when we go wrong. It is not pleasant to be disciplined. It may be painful but it is beneficial for us in the long term. The aim of God’s discipline is to help us to change our attitudes and to give up sinful behavior.

May God help us to be willing to be humble   and to listen to the correction which God gives us through The Bible and through His servants. 

  

ALHAMISI TAREHE 17  AGOSTI 2017 ASUBUHI                              

WAEBRANIA 12:7-13

Ni kwa ajili ya kurudiwa mwastahimili; Mungu awatendea kama wana; maana ni mwana yupi asiyerudiwa na babaye? 
Basi kama mkiwa hamna kurudiwa, ambako ni fungu la wote, ndipo mmekuwa wana wa haramu ninyi, wala si wana wa halali. 
Na pamoja na hayo tulikuwa na baba zetu wa mwili walioturudi, nasi tukawastahi; basi si afadhali sana kujitia chini ya Baba wa roho zetu na kuishi? 
10 Maana ni hakika, hao kwa siku chache waliturudi kama walivyoona vema wenyewe; bali yeye kwa faida yetu, ili tuushiriki utakatifu wake. 
11 Kila adhabu wakati wake haionekani kuwa kitu cha furaha, bali cha huzuni; lakini baadaye huwaletea wao waliozoezwa nayo matunda ya haki yenye amani. 
12 Kwa hiyo inyosheni mikono iliyolegea na magoti yaliyopooza, 
13 mkaifanyie miguu yenu njia za kunyoka, ili kitu kilicho kiwete kisipotoshwe, bali afadhali kiponywe. 
 

Mungu anatupenda. Kwa sababu anatupenda anaturudi. Kurudiwa inaumiza na mara nyingi hatufurahi kurudiwa.  Lakini ni kwa faida yetu ili tuwezekuacha dhambi na kuishi maisha ambayo  yanampendeza Mungu.

Tuwe wanyenyekevu. Kama Roho Mtakatifu anatugusa na kuonyesha dhambi zetu, hata kama Mtumishi wa Mungu hata kama rafiki anatuonya, tuwe tayari kusikiliza. Tuchunguze maisha yetu na tuwe tayari kutubu dhambi zetu na kubadilisha mwenendo wetu.