Date: 
28-03-2019
Reading: 
Genesis 7:1-5 (Mwanzo 7:1-5)

THURSDAY 28TH MARCH 2019 MORNING                                    

 Genesis 7:1-5 New International Version (NIV)

1 The Lord then said to Noah, “Go into the ark, you and your whole family, because I have found you righteous in this generation. Take with you seven pairs of every kind of clean animal, a male and its mate, and one pair of every kind of unclean animal, a male and its mate, and also seven pairs of every kind of bird, male and female, to keep their various kinds alive throughout the earth. Seven days from now I will send rain on the earth for forty days and forty nights, and I will wipe from the face of the earth every living creature I have made.”

And Noah did all that the Lord commanded him.

Noah had faith in God and obeyed God. God chose him for a very special task. He was to build an ark to save his family and every kind of animal from destruction. God gave Noah detailed instructions. But it was Noah who had to do the work. He could have chosen to disobey God or he could have done the work carelessly or incompletely. But we read in verse 5 that “Noah did all that the Lord commanded him”. This is great praise for Noah. May God help us all to be faithful so that we too can be praised by God for fulfilling all our responsibilities.  

ALHAMISI TAREHE 28 MACHI 2019 ASUBUHI                              

MWANZO 7:1-5

1 Bwana akamwambia Nuhu, Ingia wewe na jamaa yako yote katika safina; kwa maana nimekuona wewe u mwenye haki mbele zangu katika kizazi hiki. 
Katika wanyama wote walio safi ujitwalie saba saba, mume na mke; na katika wanyama wasio safi wawili wawili, mume na mke. 
Tena katika ndege wa angani saba saba, mume na mke; ili kuhifadhi hai mbegu juu ya uso wa nchi yote. 
Kwa maana baada ya siku saba nitainyeshea dunia mvua, siku arobaini mchana na usiku; na kila kilicho hai nilichokifanya juu ya uso wa nchi nitakifutilia mbali. 
Nuhu akafanya kama vile Bwana alivyomwamuru. 
 
Mungu alimchagua Nuhu kwa kazi maluumu na muhimu. Mungu alimwagiza Nuhu kujenga safina kuokoa maisha ya familia yake na wanyama wa kila aina. Mungu alimpa Nuhu maelezo kamili. Lakini ni Nuhu  aliyepaswa kufanya kazi. Nuhu angeweza kukataa wito huu au kufanya kwa udhaifu na uzembe. Lakini tunasoma katika mstari wa 5 “ Nuhu akafanya kama vile Bwana alivyomwamuru”. Mungu atusaidie sisi sote tuwe waaminifu na tutekeleza vizuri wajibu wetu wote.