Date: 
16-03-2018
Reading: 
Genesis 1:1-5 (Mwanzo 1:1-5)

FRIDAY  16 TH MARCH 2018 MORNING                                    

Genesis 1:1-5  New International Version (NIV)

The Beginning

1 In the beginning God created the heavens and the earth. Now the earth was formless and empty, darkness was over the surface of the deep, and the Spirit of God was hovering over the waters.

And God said, “Let there be light,” and there was light. God saw that the light was good, and he separated the light from the darkness.God called the light “day,” and the darkness he called “night.” And there was evening, and there was morning—the first day.

God created the world out of nothing. God Himself was not created. God is Eternal. He has always existed and always will exist. He made the world and everything in it. God created the world out of nothing just by speaking the word.

Let us thank God for the beautiful world which He has made and let us take care of this world as God has commanded us.   

IJUMAA 16 MACHI 2018 ASUBUHI                                                

MWANZO 1:1-5

1Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi. 
Nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji. 
Mungu akasema, Iwe nuru; ikawa nuru. 
Mungu akaiona nuru, ya kuwa ni njema; Mungu akatenga nuru na giza. 
Mungu akaiita nuru Mchana, na giza akaliita Usiku. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku moja. 
 
Mungu ni wa milele. Mungu hana Mwanzo wala mwisho. Mungu ni mwenye enzi na uwezo wote. Mungu aliumba dunia na vitu vyote kwa kusema tu, alisema na ilikuwa. Mungu ameumba binadamu kwa mfano wake na ametupa mamlaka kutawala na kutunza uumbaji. Mungu atusaidie kutekeleza majukumu kwa uaminifu. Tufurahie na kuitunza dunia hii inayopendeza sana.