Date: 
17-10-2019
Reading: 
Galatians 3:15-22 (Wagalatia 3:15-22)

THURSDAY, 17TH OCTOBER 2019 MORNING                                           

Galatians 3:15-22 New International Version (NIV)

15 Brothers and sisters, let me take an example from everyday life. Just as no one can set aside or add to a human covenant that has been duly established, so it is in this case. 16 The promises were spoken to Abraham and to his seed. Scripture does not say “and to seeds,” meaning many people, but “and to your seed,”[i] meaning one person, who is Christ. 17 What I mean is this: The law, introduced 430 years later, does not set aside the covenant previously established by God and thus do away with the promise. 18 For if the inheritance depends on the law, then it no longer depends on the promise; but God in his grace gave it to Abraham through a promise.

19 Why, then, was the law given at all? It was added because of transgressions until the Seed to whom the promise referred had come. The law was given through angels and entrusted to a mediator. 20 A mediator, however, implies more than one party; but God is one.

21 Is the law, therefore, opposed to the promises of God? Absolutely not! For if a law had been given that could impart life, then righteousness would certainly have come by the law. 22 But Scripture has locked up everything under the control of sin, so that what was promised, being given through faith in Jesus Christ, might be given to those who believe.

The Galatians struggled with a basic question: How are we made right before God?  What is our standing before Him?  Because of some bad teaching, they answered those questions wrongly.  They thought, "We are made right before God based on what Jesus did for us, in addition to what we do for Him under the Law of Moses.

We who have believed in Jesus have the law written in our hearts, and it corresponds with what is written in the Scriptures. We do not need to struggle in keeping the law because it lives in us, and the Spirit of God enables us to live its requirements. To be among the sons of God means that we have a special relationship with God as a loving and caring Father.


ALHAMISI TAREHE 17 OKTOBA 2019 ASUBUHI  WAGALATIA 3:15-22

15 Ndugu zangu, nanena kwa jinsi ya kibinadamu. Lijapokuwa ni agano la mwanadamu, hata hivyo likiisha kuthibitika, hakuna mtu alibatilishaye, wala kuliongeza neno.
16 Basi ahadi zilinenwa kwa Ibrahimu na kwa mzao wake. Hasemi, Kwa wazao, kana kwamba ni wengi, bali kana kwamba ni mmoja, Kwa mzao wako, yaani, Kristo.
17 Nisemalo ni hili; agano lililothibitishwa kwanza na Mungu, torati iliyotokea miaka mia nne na thelathini baadaye hailitangui, hata kuibatilisha ile ahadi.
18 Kwa maana urithi ukiwa kwa sheria, hauwi tena kwa ahadi; lakini Mungu alimkirimia Ibrahimu kwa njia ya ahadi.
19 Torati ni nini basi? Iliingizwa kwa sababu ya makosa, hata aje huyo mzao aliyepewa ile ahadi; iliamriwa kwa utumishi wa malaika kwa mkono wa mjumbe.
20 Basi aliye mjumbe si mjumbe wa mmoja; bali Mungu ni mmoja.
21 Basi je! Torati haipatani na ahadi za Mungu? Hasha! Kwa kuwa, kama ingalitolewa sheria iwezayo kuhuisha, yakini haki ingalipatikana kwa sheria.
22 Lakini andiko limeyafunga yote chini ya nguvu ya dhambi, makusudi hao waaminio wapewe ile ahadi kwa imani ya Yesu Kristo.

Swali la msingi lililowasumbua Wakristo wa kanisa la Galatia lilikuwa: tunawezaje kupatanishwa na Mungu; na Je, tuna haki gani mbele zake?  Kwa sababu ya mafundisho potofu, walijibiwa kimakosa.  Walidhani kuwa, "tunapatanishwa na Mungu kwa sababu ya kazi ya ukombozi ya Yesu Kristo, pamoja na juhudi yetu katika kuishika sheria ya Musa.

Sisi tuliomwamini Yesu Kristo sheria ya Mungu imeandikwa mioyoni mwetu, na inafanana na kile kilichoandikwa katika maandiko matakatifu. Hatuhitaji kujitahidi kuishika sheria kwa sababu inaishi ndani yetu, na kwamba Roho wa Mungu hutuwezesha kuishi sawa sawa na kile sheria inachodai. Kuwa miongoni mwa watoto wa Mungu inamaanisha kuwa tunao uhusiano wa kipekee na Mungu kama baba anayetupenda na kutujali.