Date: 
26-01-2021
Reading: 
Exodus 20:18-26

TUESDAY 26TH January 2021    MORNING                                               

Exodus 20:18-26 New International Version (NIV)

18 When the people saw the thunder and lightning and heard the trumpet and saw the mountain in smoke, they trembled with fear. They stayed at a distance 19 and said to Moses, “Speak to us yourself and we will listen. But do not have God speak to us or we will die.”

20 Moses said to the people, “Do not be afraid. God has come to test you, so that the fear of God will be with you to keep you from sinning.”

21 The people remained at a distance, while Moses approached the thick darkness where God was.

22 Then the Lord said to Moses, “Tell the Israelites this: ‘You have seen for yourselves that I have spoken to you from heaven: 23 Do not make any gods to be alongside me; do not make for yourselves gods of silver or gods of gold.

24 “Make an altar of earth for me and sacrifice on it your burnt offerings and fellowship offerings, your sheep and goats and your cattle. Wherever I cause my name to be honored, I will come to you and bless you. 25 If you make an altar of stones for me, do not build it with dressed stones, for you will defile it if you use a tool on it. 26 And do not go up to my altar on steps, or your private parts may be exposed.’

God has a good plan and purpose for you. He can part the waters and lead you through it on dry ground. So follow Him and trust Him and He will do marvelous things for you and through you.


JUMANNE TAREHE 26 JANUARY 2021     ASUBUHI                             

KUTOKA 20:18-26

18 Watu wote wakaona umeme na ngurumo na sauti ya baragumu, na ule mlima kutoka moshi; na watu walipoona hayo wakatetemeka, wakasimama mbali.
19 Wakamwambia Musa, Sema nasi wewe, nasi tutasikia, bali Mungu asiseme nasi, tusije tukafa.
20 Musa akawaambia watu, Msiogope, maana Mungu amekuja ili awajaribu, na utisho wake uwe mbele yenu, ili kwamba msifanye dhambi.
21 Basi hao watu wakasimama mbali, naye Musa akalikaribia lile giza kuu Mungu alipokuwapo.
22 Bwana akamwambia Musa, Waambie wana wa Israeli hivi, Ninyi wenyewe mmeona ya kuwa nimenena nanyi kutoka mbinguni.
23 Msifanye miungu mingine pamoja nami; miungu ya fedha, wala miungu ya dhahabu, msijifanyie.
24 Utanifanyia madhabahu ya udongo, nawe utatoa dhabihu zako juu yake; sadaka za kuteketezwa, na sadaka za amani, kondoo zako, na ng'ombe zako, kila mahali nitakapotia ukumbusho wa jina langu, hapo ndipo nitakapokujilia na kukubarikia.
25 Nawe ukinifanyia madhabahu ya mawe, hutaijenga ya mawe yaliyochongwa; kwa kuwa ukiwa wewe umetumia chombo chako katika kuichonga umeitia unajisi.
26 Tena hutapanda kwenda madhabahuni kwangu kwa daraja, uchi wako usidhihirike juu yake.

Mungu ana mpango na kusudi jema kwa ajili yako. Anao uwezo hata wa kugawanya bahari ili upite katika nchi kavu. Hivyo, mfuate na kumwamini, naye atatenda mambo ya ajabu kwa ajili yako; na kwa kupitia maisha yako.