Date: 
26-02-2018
Reading: 
Exodus 1:8-14 NIV (Kutoka 1:8-14)

MONDAY 26TH FEBRUARY 2018 MORNING                      

Exodus 1:8-14 New International Version (NIV)

Then a new king, to whom Joseph meant nothing, came to power in Egypt. “Look,” he said to his people, “the Israelites have become far too numerous for us. 10 Come, we must deal shrewdly with them or they will become even more numerous and, if war breaks out, will join our enemies, fight against us and leave the country.”

11 So they put slave masters over them to oppress them with forced labor, and they built Pithom and Rameses as store cities for Pharaoh.12 But the more they were oppressed, the more they multiplied and spread; so the Egyptians came to dread the Israelites 13 and worked them ruthlessly. 14 They made their lives bitter with harsh labor in brick and mortar and with all kinds of work in the fields; in all their harsh labor the Egyptians worked them ruthlessly.

This week we are thinking about the problem of violence and discrimination. We see how the Israelites were oppressed by their Egyptian masters. They were made to work extremely hard in the hot sun.

Even today many people are mistreated. This occurs in many countries. Let us think what we can do to stand against all such bad treatment, and also examine our own lives to make sure that we are not ill-treating other people.

JUMATATU TAREHE 26 FEBRUARI 2018 ASUBUHI     

KUTOKA 1:8-14

Basi akainuka mfalme mpya kutawala Misri, asiyemjua Yusufu. 
Akawaambia watu wake, Angalieni, watu wa wana wa Israeli ni wengi tena wana nguvu kuliko sisi. 
10 Haya! Na tuwatendee kwa akili, wasije wakaongezeka; tena, ikitokea vita, wao nao wasije wakashikamana na adui zetu na kupigana nasi, na kutoka katika nchi hii. 
11 Basi wakaweka wasimamizi juu yao wawatese kwa mizigo yao. Nao wakamjengea Farao miji ya kuwekea akiba, Pithomu na Ramesesi. 
12 Lakini kwa kadiri ya walivyowatesa ndivyo walivyoongezeka na kuzidi kuenea. Nao walichukiwa kwa sababu ya wana wa Israeli. 
13 Wamisri wakawatumikisha wana wa Israeli kwa ukali; 
14 wakafanya maisha yao kuwa uchungu kwa kazi ngumu; kazi ya chokaa na ya matofali, na kila namna ya kazi ya mashamba; kwa kazi zao zote walizowatumikisha kwa ukali. 

Wiki hii tunatafakari kuhusu shida ya ukatili. Hapo juu tunasoma jinsi Waisraeli kule Misri waliteswa na wanyapara wao Wamisri. Walitumikishwa kazi nzito sana bila huruma.

Watu wengi katika nchi mbalimbali wanateseka. Tujitahidi kutetea wanyonge. Tujichunguze kuona kama sisi tunawatendea vibaya watu wengine.