Date: 
04-08-2017
Reading: 
Deuteronomy 7:12-18 NIV (KUMBUKUMBU LA TORATI 7:12-18)

FRIDAY  4TH AUGUST 2017 MORNING                                

Deuteronomy 7:12-18  New International Version (NIV)

12 If you pay attention to these laws and are careful to follow them, then the Lord your God will keep his covenant of love with you, as he swore to your ancestors. 13 He will love you and bless you and increase your numbers. He will bless the fruit of your womb, the crops of your land—your grain, new wine and olive oil—the calves of your herds and the lambs of your flocks in the land he swore to your ancestors to give you.14 You will be blessed more than any other people; none of your men or women will be childless, nor will any of your livestock be without young.15 The Lord will keep you free from every disease. He will not inflict on you the horrible diseases you knew in Egypt, but he will inflict them on all who hate you. 16 You must destroy all the peoples the Lord your God gives over to you. Do not look on them with pity and do not serve their gods, for that will be a snare to you.

17 You may say to yourselves, “These nations are stronger than we are. How can we drive them out?” 18 But do not be afraid of them; remember well what the Lord your God did to Pharaoh and to all Egypt.

 

God is faithful to us. He shows us His love in so many ways. We need also to honour, love and obey God. This will be pleasing to God and a blessing to us and to other people.

We only bring problems to ourselves and other people by rebelling against God and trying to live in our own way.

We know that we cannot earn our salvation by works but only by trusting in Jesus Christ as our Lord and savior but our behavior is still very important. Let us not play with sin.

Be humble and ask God to guide you in your life.

IJUMAA TAREHE 4 AGOSTI 2017 ASUBUHI     

KUMBUKUMBU LA TORATI 7:12-18

 

12 Na itakuwa, kwa sababu mwazisikiliza hukumu hizi, na kuzishika na kuzitenda, basi Bwana, Mungu wako, atakutimilizia agano na rehema aliyowaapia baba zako; 
13 naye atakupenda na kukubarikia na kukuongeza tena ataubarikia uzao wa tumbo lako, na uzao wa nchi yako, nafaka zako na divai yako, na mafuta yako, maongeo ya ng'ombe zako, na wadogo wa kondoo zako, katika nchi aliyowaapia baba zako kuwa atakupa. 
14 Utabarikiwa kuliko mataifa yote; hakutakuwa na mtu mume wala mke aliye tasa kati yenu; wala kati ya wanyama wenu wa mifugo. 
15 Na Bwana atakuondolea ugonjwa wote; wala hatatia juu yako maradhi yo yote mabaya uyajuayo ya Misri, lakini atayaweka juu ya wote wakuchukiao. 
16 Nawe angamiza mataifa yote atakayokupa Bwana, Mungu wako; jicho lako lisiwahurumie, wala usiitumikie miungu yao; kwani litakuwa ni mtego kwako jambo hilo. 
17 Nawe kama ukisema moyoni mwako, Mataifa haya ni mengi kunipita mimi; nitawatoaje katika milki yao? 
18 Usiwaogope; kumbuka sana Bwana, Mungu wako, alivyomfanya Farao na Misri yote; 
 

Mungu ni mwaminifu kwetu. Mungu anaonyesha upendo wake kwetu kwa njia nyingi. Sisi tunapaswa kuitikia kwa kumpenda, kumheshimu na kumtii Mungu wetu. Tuwe na mawazo, maneno na matendo mema. Kufanya hivi itampendeza Mungu na binadamu wenzetu na itatuletea furaha na amani maishani.

Hatuokolewi kwa njia ya matendo yetu bali kwa imani katika Yesu Kristo, lakini hatupaswi kuchezea dhambi. Tubu dhambi zako na kukubali kuongozwa na Mungu katika maisha yako kila siku.