Date: 
20-03-2019
Reading: 
Daniel 3:19-23

WEDNESDAY 20TH MARCH 2019

Daniel 3:19-23 New International Version (NIV)

19 Then Nebuchadnezzar was furious with Shadrach, Meshach and Abednego, and his attitude toward them changed. He ordered the furnace heated seven times hotter than usual 20 and commanded some of the strongest soldiers in his army to tie up Shadrach, Meshach and Abednego and throw them into the blazing furnace. 21 So these men, wearing their robes, trousers, turbans and other clothes, were bound and thrown into the blazing furnace. 22 The king’s command was so urgent and the furnace so hot that the flames of the fire killed the soldiers who took up Shadrach, Meshach and Abednego, 23 and these three men, firmly tied, fell into the blazing furnace.

The above verses are part of the story about three young men who believed in the true God of Israel, and stood up for their faith against a cruel King. In keeping our faith we will come upon many testing situations that will put us at cross roads with our faith. But we must remain strong whatever the case, praying to God to help us through.

JUMATANO TAREHE 20 MACHI 2019

Daniel 3:19-23

19 Ndipo Nebukadreza akajaa ghadhabu, na sura ya uso wake ikabadilika juu ya Shadraka, na Meshaki, na Abednego, basi akatoa amri watie moto ile tanuru mara saba kuliko desturi yake ya kutiwa moto. 
20 Kisha akawaamuru baadhi ya watu mashujaa wa jeshi lake kuwafunga Shadraka, na Meshaki, na Abednego, na kuwatupa katika ile tanuru iliyokuwa ikiwaka moto. 
21 Basi watu hao wakafungwa, hali wamevaa suruali zao, na kanzu zao, na joho zao, na mavazi yao mengine, wakatupwa katikati ya ile tanuru iliyokuwa ikiwaka moto. 
22 Basi kwa sababu amri ya mfalme ilikuwa ni kali, na ile tanuru ilikuwa ina moto sana, mwako wa ule moto ukawaua wale watu waliowashika Shadraka, na Meshaki, na Abednego. 
23 Na watu hao watatu, Shadraka, na Meshaki, na Abednego, wakaanguka, hali wamefungwa, katikati ya ile tanuru iliyokuwa inawaka moto. 

Aya zilizo hapo juu ni sehemu ya hadithi kuhusu vijana watatu waliomwamini Mungu wa kweli wa Israeli, na kusimama kwa imani yao dhidi ya Mfalme mkatili. Katika kuishi imani yetu tutapata majaribu mengi ambayo yatatuweka njia panda. Lakini tunapaswa kusimama imara huku tukiwomba Mungu atusaidie kuvuka salama.