Date: 
05-01-2022
Reading: 
2Peter 1:12-15

Jumatano asubuhi tarehe 05.01.2022

2 Petro 1:12-15

12 Kwa hiyo nitakuwa tayari kuwakumbusha hayo siku zote, ijapokuwa mnayajua na kuthibitishwa katika kweli mliyo nayo.

13 Nami naona ni haki, maadamu nipo mimi katika maskani hii, kuwaamsha kwa kuwakumbusha.

14 Nikijua kwamba kule kuwekea mbali maskani yangu kwaja upesi, kama Bwana wetu Yesu Kristo alivyonionyesha.

15 Walakini nitajitahidi, kwamba kila wakati baada ya kufariki kwangu mpate kuyakumbuka mambo hayo.

Waliomngojea Mwokozi wamuona;

Tumesoma Petro akiandika kuhusu ujio wa Yesu, akisema anakumbusha kuhusu yale tuyajuayo. Yaani tunajua kuwa Yesu atarudi, hivyo Petro anatusihi njia zetu kuwa sawa pasipo kusahau ujio wa Kristo.

Tunapokumbushwa kurudi kwa Yesu, tunajiandaaje? Tunapotafakari juu ya kumngoja Bwana, tunamngoja vipi? 

Tunamngoja Bwana kwa kudumu katika imani bila kutetereka. Tunamngoja Bwana kwa kusoma neno lake na kusali ili tubaki katika njia sahihi. Tunamngoja Bwana kwa kufanya yaliyo mapenzi yake, maana hicho ni kielelezo cha imani yetu kwake.

Tuendelee kumngoja Yesu kwa imani tukitenda yatupasayo kuelekea uzima wa milele.

Jumatano njema.