Date: 
05-10-2019
Reading: 
2Kings 14:1-16 (2Wafalme 14:1-16)

Saturday 5th October 2019 Morning                                                              
2 Kings 14:1-6 New International Version (NIV)

14 In the second year of Jehoash[a] son of Jehoahaz king of Israel, Amaziah son of Joash king of Judah began to reign. 2 He was twenty-five years old when he became king, and he reigned in Jerusalem twenty-nine years. His mother’s name was Jehoaddan; she was from Jerusalem. 3 He did what was right in the eyes of the Lord, but not as his father David had done. In everything he followed the example of his father Joash. 4 The high places, however, were not removed; the people continued to offer sacrifices and burn incense there.
5 After the kingdom was firmly in his grasp, he executed the officials who had murdered his father the king. 6 Yet he did not put the children of the assassins to death, in accordance with what is written in the Book of the Law of Moses where the Lord commanded: “Parents are not to be put to death for their children, nor children put to death for their parents; each will die for their own sin.”[b]

“Learn to do right; seek justice. Defend the oppressed. Take up the cause of the fatherless; plead the case of the widow” (Isaiah 1:17).
 If we do not remove evil influences from our lives, we place ourselves and our families in spiritual danger.


JUMAMOSI TAREHE 5 OKTOBA 2019 ASUBUHI                                                             
2 WAFALME 14:1-6

1 Katika mwaka wa pili wa Yehoashi mwana wa Yehoahazi mfalme wa Israeli Amazia mwana wa Yoashi mfalme wa Yuda alianza kutawala.
2 Naye alikuwa na umri wa miaka ishirini na mitano alipoanza kutawala; akatawala miaka ishirini na kenda katika Yerusalemu; na jina la mamaye aliitwa Yehoadani wa Yerusalemu.
3 Akafanya yaliyo mema machoni pa Bwana, ila si kama babaye Daudi; akafanya kama yote aliyoyafanya baba yake Yoashi.
4 Walakini mahali pa juu hapakuondolewa; watu wakaendelea kutoa dhabihu na kufukiza uvumba katika mahali pa juu.
5 Ikawa, mara ufalme ulipokuwa imara mkononi mwake, aliwaua watumishi wale waliomwua mfalme baba yake;
6 ila hakuwaua watoto wa hao wauaji; kama ilivyoandikwa katika kitabu cha torati ya Musa, kama alivyoamuru Bwana, akisema, Mababa wasife kwa makosa ya wana, wala wana wasife kwa makosa ya mababa; lakini kila mtu atakufa kwa kosa lake mwenyewe.

“Jifunzeni kutenda mema; takeni hukumu na haki; wasaidieni walioonewa; mpatieni yatima haki yake; mteteeni mjane” (Isaya 1:17).
Tusipoondoa nguvu ya uovu katika maisha yetu, tunajiweka katika hatari ya kiroho, sisi pamoja na watoto wetu.