Date: 
04-07-2017
Reading: 
2 Timothy 1:3-7 NIV {2Timotheo 1:3-7}

TUESDAY 4TH JULY 2017 MORNING                                     

2 Timothy 1:3-7 New International Version (NIV)

Thanksgiving

I thank God, whom I serve, as my ancestors did, with a clear conscience, as night and day I constantly remember you in my prayers.Recalling your tears, I long to see you, so that I may be filled with joy.I am reminded of your sincere faith, which first lived in your grandmother Lois and in your mother Eunice and, I am persuaded, now lives in you also.

Appeal for Loyalty to Paul and the Gospel

For this reason I remind you to fan into flame the gift of God, which is in you through the laying on of my hands. For the Spirit God gave us does not make us timid, but gives us power, love and self-discipline.

The Apostle Paul wrote this letter to the young Pastor Timothy. He wrote to encourage him in his faith and his ministry. Notice how Timothy’s Grandmother had passed on her faith to her daughter and that both these women had nurtured Timothy in his faith.

Thank God for those people who lead you to Christ and who have helped and encouraged you in your spiritual life. Think about whom you can mentor.

JUMANNE TAREHE 4 JULAI 2017 ASUBUHI                        

2 TIMOTHEO 1:3-7

Namshukuru Mungu, nimwabuduye kwa dhamiri safi tangu zamani za wazee wangu, kama vile nikukumbukavyo wewe daima, katika kuomba kwangu usiku na mchana. 
Nami natamani sana kukuona, nikiyakumbuka machozi yako, ili nijae furaha; 
nikiikumbuka imani uliyo nayo isiyo na unafiki, ambayo ilikaa kwanza katika bibi yako Loisi, na katika mama yako Eunike, nami nasadiki wewe nawe unayo. 
Kwa sababu hiyo nakukumbusha, uichochee karama ya Mungu, iliyo ndani yako kwa kuwekewa mikono yangu. 
Maana Mungu hakutupa roho ya woga, bali ya nguvu na ya upendo na ya moyo wa kiasi. 

Mtume Paulo aliandika Waraka huu kwa Mchungaji kijana Timotheo. Aliandika ili amtie moyo katika imani yake na huduma yake. Paulo anaelezea jinsi bibi na mama wa Timotheo walimlea kiroho.

Mshukuru Mungu kwa watu walikuleta wewe kwa Yesu na wamekulea kiroho. Tafakari jinsi unavyoweza kusaidia wengine kiroho.