Date: 
17-03-2022
Reading: 
2 Samweli 1:8-12

Hii ni Kwaresma 
Alhamisi asubuhi tarehe17.03.2022

2 Samweli 1:8-12
8 Akaniambia, U nani wewe? Nikamjibu, Mimi ni Mwamaleki.
9 Akaniambia, Tafadhali simama karibu nami, ukaniue, maana shida imenipata; kwa sababu roho yangu ingali hai ndani yangu.
10 Basi, nikasimama karibu naye, nikamwua, kwa sababu nalijua hakika ya kuwa hawezi kupona baada ya kuanguka; kisha nikaitwaa ile taji iliyokuwa kichwani mwake, na kikuku kilichokuwa mkononi mwake, nami nimevileta hapa kwa bwana wangu.
11 Ndipo Daudi akashika nguo zake akazirarua na kadhalika watu wote waliokuwa pamoja naye;
12 wakaomboleza, wakalia, wakafunga hata jioni, kwa ajili ya Sauli, na kwa ajili ya Yonathani mwanawe, na kwa ajili ya watu wa Bwana na kwa ajili ya nyumba ya Israeli; kwa sababu wameanguka kwa upanga.

Tupinge ukatili;

Asubuhi hii tunamsoma kijana aliyetokea mbele ya Daudi akikiri kumuua Sauli na mwanae Yonathani! Kitendo ambacho kilimuumiza sana Daudi, hadi kuomboleza. Daudi hakuwa tayari kuona Sauli akiuawa, japokuwa alikuwa kinyume naye, maana Sauli hakufurahishwa na ushujaa wa Daudi.

Imefikia hatua ya baadhi yetu  kufanya uovu hadharani! Hatuheshimu sheria za nchi, wala hofu ya Mungu haipo. Jambo hili halikubaliki kwa waaminio, hata wasioamini, maana hakuna mwenye haki ya kutesa na kuangamiza wengine. Tutumie nafasi zetu vema kwa manufaa ya familia zetu, nchi na Kanisa kwa ujumla.


Siku njema.