Date: 
01-07-2021
Reading: 
2 Kings 6:18-25 (Wafalme)

THURSDAY 1ST JULY 2021    MORNING                                               

2 Kings 6:18-25 New International Version (NIV)

18 As the enemy came down toward him, Elisha prayed to the Lord, “Strike this army with blindness.” So he struck them with blindness, as Elisha had asked.

19 Elisha told them, “This is not the road and this is not the city. Follow me, and I will lead you to the man you are looking for.” And he led them to Samaria.

20 After they entered the city, Elisha said, “Lord, open the eyes of these men so they can see.” Then the Lord opened their eyes and they looked, and there they were, inside Samaria.

21 When the king of Israel saw them, he asked Elisha, “Shall I kill them, my father? Shall I kill them?”

22 “Do not kill them,” he answered. “Would you kill those you have captured with your own sword or bow? Set food and water before them so that they may eat and drink and then go back to their master.” 23 So he prepared a great feast for them, and after they had finished eating and drinking, he sent them away, and they returned to their master. So the bands from Aram stopped raiding Israel’s territory.

God is our all-sufficient resource in times of trial; and, that prayer is our means of access to the all-sufficient God.

Since God is our all-sufficient resource, we should pray and not panic when trials come.


ALHAMISI TAREHE 1 JULAI 2021     ASUBUHI                                 

2 WAFALME 6:18-25

18 Na walipomtelemkia Elisha akamwomba Bwana, akasema, Uwapige, nakusihi, watu hawa kwa upofu. Akawapiga kwa upofu sawasawa na neno la Elisha.
19 Elisha akawaambia, Njia hii siyo, na mji huu sio, nifuateni mimi, nami nitawapeleka kwa mtu yule mnayemtafuta. Akawapeleka Samaria.
20 Hata walipokwisha kuingia Samaria, Elisha akasema, Bwana wafumbue macho watu hawa, wapate kuona. Bwana akawafumbua macho wakaona; kumbe! Walikuwa katikati ya Samaria.
21 Naye mfalme wa Israeli alipowaona, akamwambia Elisha, Ee baba yangu, niwapige? Niwapige?
22 Akamjibu, Usiwapige; je! Ungetaka kuwapiga watu ambao umewatwaa mateka kwa upanga wako na uta wako? Weka chakula na maji mbele yao, wapate kula na kunywa, na kwenda kwa bwana wao.
23 Basi akawaandalia chakula tele; nao walipokwisha kula na kunywa, akawaacha, wakaenda zao kwa bwana wao. Na vikosi vya Shamu havikuja tena katika nchi ya Israeli.


Mungu ndiye anayeweza kututosheleza katika nyakati za shida; na kwamba maombi ndiyo njia pekee ya kumfikia Mungu huyu aliye mtoshelevu.

Kwa kuwa Mungu ndiye anayetutosheleza, tunapaswa kuomba, wala tusichanganyikiwe pale shida na majaribu yanapotujia.