Date: 
21-12-2016
Reading: 
1 John 1:1-4; Wed 21st Dec

WEDNESDAY 21ST DECEMBER 2016 MORNING                           

1 John 1:1-4  New International Version (NIV)

The Incarnation of the Word of Life

1 That which was from the beginning, which we have heard, which we have seen with our eyes, which we have looked at and our hands have touched—this we proclaim concerning the Word of life. The life appeared; we have seen it and testify to it, and we proclaim to you the eternal life, which was with the Father and has appeared to us. We proclaim to you what we have seen and heard, so that you also may have fellowship with us. And our fellowship is with the Father and with his Son, Jesus Christ. We write this to make our[a] joy complete.

Footnotes:

  1. 1 John 1:4 Some manuscripts your 

The Apostle John begins his first letter in a similar way to that in which he begins his Gospel. He talks about the beginning. He talks about the fact that Jesus Christ has always existed even though He came down to earth, born as a human being into the history of mankind. John proclaims that he is an eyewitness to Jesus Christ.

What is your testimony about Jesus Christ in your life?

JUMATANO TAREHE 21 DISEMBA 2016 ASUBUHI                       

1 YOHANA 1:1-4

1 Lile lililokuwako tangu mwanzo, tulilolisikia, tuliloliona kwa macho yetu, tulilolitazama, na mikono yetu ikalipapasa, kwa habari ya Neno la uzima; 
2 (na uzima huo ulidhihirika, nasi tumeona, tena twashuhudia, na kuwahubiri ninyi ule uzima wa milele, uliokuwa kwa Baba, ukadhihirika kwetu); 
3 hilo tuliloliona na kulisikia, twawahubiri na ninyi; ili nanyi pia mpate kushirikiana nasi: na ushirika wetu ni pamoja na Baba, na pamoja na Mwana wake Yesu Kristo. 
4 Na haya twayaandika, ili furaha yetu itimizwe. 


Lugha ya mwanzo wa Waraka huu wa kwanza wa Yohana inafanana na ile katika mistari ya kwanza ya Injili ya Yohana. Anaeleza kuhusu Yesu Kristo aliyekuwepo tangu mwanzo. Yesu ni wa milele. Yesu alikuwa na Baba yake mbinguni kabla kuzaliwa kule Bethlehem. Yohana anatoa ushuhuda wake jinsi alimwona Yesu na kusikia mafundisho yake.

Ushuhuda wako kuhusu Yesu ni nini?