Date: 
26-05-2020
Reading: 
 Lamentations 3:52-57 Maombolezo 3:52-57

TUESDAY 26TH MAY 2020    MORNING                                            

 Lamentations 3:52-57 New International Version (NIV)

52 Those who were my enemies without cause
    hunted me like a bird.
53 They tried to end my life in a pit
    and threw stones at me;
54 the waters closed over my head,
    and I thought I was about to perish.

55 I called on your name, Lord,
    from the depths of the pit.
56 You heard my plea: “Do not close your ears
    to my cry for relief.”
57 You came near when I called you,
    and you said, “Do not fear.”

God never hides His ear from our cry, which express, as words could not do, the deep pain and desire of the heart. If we cannot speak, we can cry, and then still God can interpret all.

“Do not fear”. How powerful is this word when spoken by the Spirit of the Lord to an unhappy heart. To every mourner we may say, on the authority of God, Fear not! God will plead your cause, and redeem your soul.


JUMANNE TAREHE 26 MEI 2020     ASUBUHI                                            

MAOMBOLEZO 3:52-57

52 Walio adui zangu bila sababu Wameniwinda sana kama ndege;
53 Wameukatilia mbali uhai wangu gerezani, Na kutupa jiwe juu yangu.
54 Maji mengi yalipita juu ya kichwa changu, Nikasema, Nimekatiliwa mbali.
55 Naliliitia jina lako, Bwana, kutoka lile shimo Liendalo chini kabisa.
56 Ukaisikia sauti yangu; usifiche sikio lako Ili usisikie pumzi yangu, kwa kilio changu.
57 Ulinikaribia siku ile nilipokulilia; Ukasema, Usiogope.

Mungu kamwe hawezi kuficha sikio lake hata asisikie kilio chetu, kinachoeleza maumivu na haja za mioyo yetu kuliko ambavyo maneno yetu yangeweza. Ikiwa hatuwezi kuongea, tunaweza kulia, na kisha Mungu akaelewa hitaji letu.

Ni jinsi gani lilivyo na nguvu neno hili “Usiogope”, linapotamkwa na Roho wa Bwana kwa moyo wenye huzuni. Kwa kila mwenye kuomboleza Tunaweza kusema, kwa mamlaka ya Mungu; Usiogope! Mungu atakushindia katika shida yako, na kuikomboa nafsi yako.