Date: 
29-01-2026
Reading: 
1 Petro 1:13-15

Alhamisi asubuhi tarehe 29.01.2026

1 Petro 1:13-15

13 Kwa hiyo vifungeni viuno vya nia zenu, na kuwa na kiasi; mkiitumainia kwa utimilifu ile neema mtakayoletewa katika ufunuo wake Yesu Kristo.

14 Kama watoto wa kutii msijifananishe na tamaa zenu za kwanza za ujinga wenu;

15 bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote;

Yesu ajidhihirisha katika utukufu wake;

Ni wito wa kuishi maisha ya utakatifu kama Petro anavyoandika. Analiita Kanisa kufunga viuno vya nia zao, kuwa na kiasi, kwa kuutumainia utimilifu wa neema itokayo katika ufunuo wake Yesu Kristo. Petro analisihi Kanisa kuacha tamaa za ujinga na kuwa watakatifu kama yeye aliyewaita.

Petro analiita Kanisa kuishi kwa mfano wa Yesu Kristo. Yaani anawaita watu kumwamini Yesu na kuishi kwa kumfuata yeye. Kumbe nasi tuziache tamaa za dunia, tumtazame na kumfuata Yesu aliyetuita, ili tuwe watakatifu kama yeye aliyetuita. Amina

Siku njema

 

Heri Buberwa