DAYOSISI YA MASHARIKI NA PWANI

MATANGAZO YA USHARIKA

TAREHE 25 JANUARI, 2026

SIKU YA BWANA YA MWISHO KATIKA MAJIRA YA UFUNUO

NENO LINALOTUONGOZA NI

YESU AJIDHIHIRISHA KATIKA UTUKUFU WAKE

1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.

2. Wageni: Hakuna mgeni aliyetufikia na cheti.

3. Matoleo ya Tarehe 18/01/2026

Jumla - Tshs 16,381,350/= Rwanda FR 5,000/=

MATOLEO KATIKATI YA WIKI

Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.

NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:

- 0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT

Lipa namba M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL

4. Mahudhurio ya ibada za tarehe 18/01/2026 ni Washarika 883 na Sunday School 200

5. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4:30 asubuhi. Vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Ibada ya asubuhi saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada ya mchana saa 7.00 mchana. Ijumaa saa 11.00 jioni tuna kipindi cha Maombi na Maombezi, ambapo tunajifunza neno la Mungu na kupata muda wa kutosha wa maombi. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front Cathedral.

6. Kitenge chetu kipya cha Kiharaka kinapatikana kwenye duka letu la vitabu kwa bei ya Tsh. 40,000/=.

7. Leo tarehe 25.01.2026 tutashiriki chakula cha Bwana. Washarika karibuni.

8. Jumapili ijayo tarehe 01/02/2026 tutamtolea Mungu fungu la kumi. Washarika tujiandae.

9. Washarika ambao bado hawajaza fomu za mwaka huu wachukue fomu kwa wazee wa Kanisa, vile vile fomu zitapatikana ofisini katikati ya wiki. Kwa washarika wapya wafike ofisini ili waweze kupewa utaratibu wa kupata bahasha.

10. Kwaya ya Agape inawashukuru uongozi wa kanisa, Walezi kamati ya malezi na washarika wote waliowashika mkono katika Huduma wanayofanya kila mwaka pale MOI kwa watoto wenye mtindio wa ubongo kwa kuwalipia bima na mahitaji mbalimbali. Wanarudi tena kwenu washarika mwaka huu tukiendelea na huduma hii pale Muhimbili na tunatarajia kufika pia Ocean road hospital kuwasaidia watoto na wakubwa wanaohitaji matibabu kwa kadri Mungu wetu na washarika mtakavyotuwezesha. Tunaomba mtakaoweza kuleta mahitaji kama mafuta ya kujipaka,dawa za meno,sabuni ya kufulia au kuogea ,maji ya kunywa pampas,nguo nzuri za watoto na wakubwa lakini pia kulipia watoto Bima ya Afya ambayo kwa mtoto mmoja ni Tsh 150,000. Unaweza kuchangia kupitia kwenye Acc ya Maendeleo Bank No 013874006021 jina Agape Evangelical Singer Azania Front Au kwa njia ya simu Yaani M-Pesa namba 0767214441 jina Janice Kaisi. Kwa maelezo zaidi unaweza kuwaona viongozi wa kwaya ya Agape. Mungu akubariki sana.

11. Idara ya Wanawake na Watoto imeandaa ibada maalum ya kusifu na kuabudu jumamosi ijayo tarehe 31/01/2026 kuanzia saa nne asubuhi katika Usharika wa Kipawa. Hivyo safari itaanza saa tatu kamili hapa Kanisani. Wanawake wanaombwa kufika kwa wakati. Sare ni Kitenge cheupe cha DMP.

12. Jumanne ijayo tarehe 27/01/2026 saa 11.00 jioni kutakuwa na kikao cha Kamati ya utendaji ya Baraza la wazee na Alhamisi tarehe 29/01/2026 saa 11.00 jioni kikao cha Baraza la Wazee. Wajumbe wote mnaombwa kuhudhuria bila kukosa na kufika kwa wakati.

13. SHUKRANI: Jumapili ijayo tarehe 01/02/2026 familia mbili zitamshukuru Mungu. Katika ibada ya Kwanza saa 1.00 asubuhi,

  • Kamati ya usafi hapa Kanisani watamshukuru Mungu kwa wema wake na kuwapigania kwa kipindi cha Mwaka 2025.

Neno: Zaburi 92:1-5, Wimbo: TMW 259

  • Mzee Stephen Emanuel Matee, atamshukuru Mungu kwa Neema, wema na mambo mengi aliyomtendea maishani mwake ikiwa ni pamoja na kufikisha miaka themanini (80) juzi ijumaa tarehe 30/01/2026/.

Neno: Zaburi 103:1-5, Wimbo: TMW 270

14. NDOA: NDOA ZA WASHARIKA

- KWA MARA YA KWANZA TUNATANGAZA NDOA YA TAREHE 14/02/2026. NDOA HII ITAFUNGWA KKKT MOSHI MJINI KATI YA

  • Bw. Cliffson Lord Macha na Bi Karen Edmund Maeda

Matangazo mengine yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo karibu na duka letu la vitabu.

15. IBADA ZA NYUMBA KWA NYUMBA

- Upanga: Kwa Mama Ndossi

- Mjini kati: Hapa usharikani saa moja kamili asubuhi

- Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo: Kwa Mzee Evatt Kuzilwa

- Tegeta, Kunduchi, Bahari Beach, Ununio: Kwa Bwana na Bibi Nyamajeje Buchanagandi

16. habari na taarifa nyingine, tembelea tovuti yetu ya Azania front. org, pia tupo Facebook na Instagram.

17. Zamu: Zamu za wazee ni kundi la Pili.

  Na huu ndiyo mwisho wa matangazo yetu, Bwana ayabariki.