Date:
06-11-2025
Reading:
Mithali 10:7
Alhamisi asubuhi tarehe 06.11.2025
Mithali 10:7
Kuwakumbuka wenye haki huwa na baraka; Bali jina la mtu mwovu litaoza.
Tunaitwa kuwa wenyeji wa mbinguni;
Katika uandishi wake, Suleimani anataja sana "wenye/mwenye haki". Suleimani anasisitiza sana watu kuishi maisha ya haki. Haki anayoisema Suleimani ni ile inayopatika kwa kuishi katika Bwana, maana ndiye mwenye haki kwao wamwitao. Kwa kusisitiza hilo, katika mstari tuliosoma Suleimani anasema jina la mtu mwovu litaoza.
Suleimani anashauri kuachana na uovu ili jina lisioze. Ushauri huu ni wa kwetu asubuhi hii, kwamba tuishi maisha ya kumpendeza Mungu ili tuhesabiwe haki atakaporudi. Tuache uovu ili majina yetu yasioze. Yaani tumwamini Yesu Kristo aliye njia ya kweli na uzima ili tuwe wenyeji wa mbinguni. Amina
Alhamisi njema
Heri Buberwa Nteboya
0784 968650
