Date: 
25-09-2025
Reading: 
2 Wakorintho 8:1-4

Alhamisi asubuhi tarehe 25.09.2025

2 Wakorintho 8:1-4

1 Tena ndugu zetu, twawaarifu habari ya neema ya Mungu, waliyopewa makanisa ya Makedonia;

2 maana walipokuwa wakijaribiwa kwa dhiki nyingi, wingi wa furaha yao na umaskini wao uliokuwa mwingi uliwaongezea utajiri wa ukarimu wao.

3 Maana nawashuhudia kwamba, kwa uwezo wao, na zaidi ya uwezo wao, kwa hiari yao wenyewe walitoa vitu vyao;

4 wakituomba sana pamoja na kutusihi kwa habari ya neema hii, na shirika hili la kuwahudumia watakatifu.

Tunaitwa kuwa mawakili wa Mungu;

Mtume Paulo anawaandikia watu wa Korintho juu ya ukarimu wa watu wa Makedonia. Paulo anaandika kwamba watu wa Makedonia walijaribiwa kwa dhiki nyingi, lakini furaha yao na umaskini wao viliwaongezea ukarimu. Yaani katikati ya dhiki na umaskini, furaha yao haikukoma. Badala yake walimtolea Mungu vitu vyao kwa hiari. 

Paulo anaonesha furaha ya watu wa Makedonia katikati ya dhiki. Ni wito kwetu kutokata tamaa katika njia ya ufuasi tukidhani Kristo ametuacha. Kristo hatuachi, bali katika hali zote sisi ndiyo tusimuache. Tunakaa kwa Kristo kwa njia ya imani, tukimtumikia na kutoa vipawa vyetu kwa uaminifu. Amina

Alhamisi njema

Heri Buberwa Nteboya 

0784 968650 

bernardina.nyamichwo@gmail.com