Date: 
24-09-2025
Reading: 
Malaki 3:7-12

Jumatano asubuhi tarehe 24.09.2025

Malaki 3:7-12

7 Tokea siku za baba zenu mmegeuka upande, mkayaacha maagizo yangu, wala hamkuyashika. Nirudieni mimi, nami nitawarudia ninyi, asema Bwana wa majeshi. Lakini ninyi mwasema, Turudi kwa namna gani?

8 Je! Mwanadamu atamwibia Mungu? Lakini ninyi mnaniibia mimi. Lakini ninyi mwasema, Tumekuibia kwa namna gani? Mmeniibia zaka na dhabihu.

9 Ninyi mmelaaniwa kwa laana; maana mnaniibia mimi, naam, taifa hili lote.

10 Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema Bwana wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la.

11 Nami kwa ajili yenu nitamkemea yeye alaye, wala hataharibu mazao ya ardhi yenu; wala mzabibu wenu hautapukutisha matunda yake kabla ya wakati wake katika mashamba, asema Bwana wa majeshi.

12 Na mataifa yote watawaiteni heri; maana mtakuwa nchi ya kupendeza sana, asema Bwana wa majeshi.

Tunaitwa kuwa mawakili wa Mungu;

Tumesoma ujumbe ambao Bwana anawaambia Israeli kwamba wanamuibia kwa kutotoa zaka, hivyo kulaaniwa. Hii ni kwa sababu waliyaacha maagizo ya Mungu, hawakuyashika. Ndipo Bwana anawaita kumrudia kwa kutolea zaka ili wamjaribu kwa njia hiyo. Hapo anawaahidi baraka na kuwahakikishia ulinzi katika maisha yao yote na mali zao.

Ujumbe huu umekuwa ukitumika na wahubiri wengi kutishia waumini kwamba wanamwibia Mungu, ni wezi! Hawatoi zaka! Miaka zaidi ya 2400 baada ya ujumbe huu bado watu wanaambiwa wezi! Sheria! Kwa mazingira na mfumo wa wakati ule ilikuwa sahihi. Hatuna sababu ya kuitana wezi, bali kuelimishana kwamba sisi ni mawakili wa Mungu, basi tumtolee mali alizotupa kwa kazi yake. Amina

Jumatano njema

Heri Buberwa Nteboya 

0784 968650 

bernardina.nyamichwo@gmail.com