Date: 
23-09-2025
Reading: 
1 Mambo ya nyakati 29:19-17

Jumanne asubuhi tarehe 23.09.2025

1 Mambo ya Nyakati 29:16-17

16 Ee Bwana, Mungu wetu, akiba hii yote tuliyoiweka, ili tukujengee nyumba kwa ajili ya jina lako takatifu, yatoka yote mkononi mwako, na yote ni yako wewe.

17 Nami najua, Mungu wangu, ya kuwa wewe wajaribu moyo, nawe wapendezwa na unyofu. Nami katika unyofu wa moyo wangu nimeyatoa haya yote kwa hiari yangu mwenyewe; nami sasa nimeona kwa furaha watu wako, waliopo hapa, wakikutolea kwa hiari yao.

Tunaitwa kuwa mawakili wa Mungu;

Somo la asubuhi ya leo ni sehemu ya shukrani ya Daudi kwa Mungu, baada ya kuwaongoza Israeli kwa matoleo ikiwa ni maandalizi ya kujenga hekalu. Daudi anampa Bwana ukuu, utukufu, kushinda, heshima, na enzi. Anaendelea kusema kuwa vitu vyote ni vya Bwana. Daudi anaonesha shukrani yeye na watu aliowaongoza kwa ajili ya shukrani. Hili linaonekana ukianzia kusoma nyuma kidogo;

1 Mambo ya Nyakati 29:13-14

13 Basi sasa, Mungu wetu, twakushukuru na kulisifu jina lako tukufu.

14 Lakini mimi ni nani, na watu wangu ni nani, hata tuweze kutoa kwa hiari hivi? Kwani vitu vyote vyatoka kwako na katika vitu vyako mwenyewe tumekutolea.

Katika somo tulilosoma Daudi anasema akiba yote waliyokuwa nayo waliiweka ili kuijenga nyumba ya Bwana kwa jina lake takatifu, na ilitoka mkononi mwake Bwana. Uhakika aliokuwa nao Daudi ni kuwa watu walimtolea Bwana kwa hiari yao. Tunakumbushwa kumtolea Bwana mali alizotupa kwa ajili ya kazi yake, maana vyote tulivyo navyo ni vya kwake. Huo ndiyo uwakili mwema. Amina

Jumanne njema 

Heri Buberwa Nteboya 

0784 968650 

bernardina.nyamichwo@gmail.com