DAYOSISI YA MASHARIKI NA PWANI
MATANGAZO YA USHARIKA
TAREHE 21 SEPTEMBA, 2025
SIKU YA BWANA YA 14 BAADA YA UTATU
NENO LINALOTUONGOZA SIKU YA LEO NI
TUNAITWA KUWA MAWAKILI WA MUNGU
1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.
2. Wageni: Hakuna mgeni aliyetufikia na cheti. Kama kuna wageni ambao ni mara yao ya kwanza kushiriki nasi wasimame ili tuwakaribishe.
3. Matoleo ya Tarehe 14/09/2025
Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.
NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:
- 0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT
Lipa namba M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL
4. Mahudhurio ya ibada ya tarehe 14/09/2025 ni Washarika 829..
5. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4:30 asubuhi. Vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Morning Glory saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada ya mchana saa 7.00 mchana. Alhamisi saa 11.00 jioni tuna kipindi cha Maombi na Maombezi, ambapo tunajifunza neno la Mungu na kupata muda wa kutosha wa maombi. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front Cathedral.
6. Kitenge chetu kipya cha Kiharaka kinapatikana hapo nje na kwenye duka letu la vitabu kwa bei ya Tsh. 40,000/=.
7. Taasisi yetu ya Moyo Jakaya Kikwete imetimiza miaka 10 tangu kuanzishwa kwake. Katika kusherekea na kuadhimisha miaka 10 hii wamelenga kuhamasisha na kuongeza ufahamu juu ya matatizo ya magonjwa ya moyo nchini kupitia makundi mbalimbali. Hivyo ili kufanikisha hili wanatupa fursa ya kufanya vipimo vya awali vya magonjwa ya moyo bila malipo kwa washarika wote kwa mwezi huu wa Septemba na Oktoba 2025 kupitia vituo vyao vilivyopo oysteray na Kawe. Mwenye kuhitaji maelezo zaidi afike ofisi za Usharika.
8. Jumapili ijayo tarehe 28/09/2025 ni sikukuu ya Mikaeli na watoto. Hivyo ibada zote zitaongozwa na watoto wakishirikiana na wazee kundi la Kwanza. Aidha siku ya Jumamosi tarehe 27/09/2025 watoto watakuwa na michezo mbalimbali hapa kanisani kuanzia saa 3.00 asubuhi mpaka saa 10.00 jioni. Washarika tuendelee kuombea sikukuu hii ya watoto wetu.
9. Familia ya Bwana na Bibi Anania Mkota wamepata zawadi ya mtoto wa kiume jumatano tarehe 17/09/2025. Baba, Mama na mtoto wanaendelea vizuri.
10. NDOA: HAKUNA NDOA ZA WASHARIKA
Lakini matangazo mengine ya Ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo karibu na duka letu la vitabu.
11. IBADA ZA NYUMBA KWA NYUMBA
- Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo: Kwa Mama Mamkwe
- Upanga: Kwa Bwana na Bibi Frank Shuma
- Tegeta, Kunduchi, Bahari Beach, Ununio: Kwa Bwana na Bibi Albert Olotu
- Kinondoni: Kwa ………………………….
- Mjini kati: Itakuwa hapa Kanisani jumamosi saa moja kamili asubuhi
- Oysterbay/Masaki: Kwa …………………………………………..
- Ilala, Chang’ombe, Buguruni: Kwa Bw & Bibi Kelvin Matandiko
- Kawe,Mikocheni, Mbezi Beach: Kwa Bwana na Bibi Phocus Lasway ,
12. Kwa habari na taarifa nyingine, tembelea tovuti yetu ya Azania front.
org, pia tupo Facebook na Instagram.
13. Zamu: Zamu za wazee ni Kundi la Pili.
Na huu ndiyo mwisho wa matangazo yetu, Bwana ayabariki.