Date:
22-09-2025
Reading:
1Timotheo 6:17-19
Jumatatu asubuhi tarehe 22.09.2021
1 Timotheo 6:17-19
17 Walio matajiri wa ulimwengu wa sasa uwaagize wasijivune, wala wasiutumainie utajiri usio yakini, bali wamtumaini Mungu atupaye vitu vyote kwa wingi ili tuvitumie kwa furaha.
18 Watende mema, wawe matajiri kwa kutenda mema, wawe tayari kutoa mali zao, washirikiane na wengine kwa moyo;
19 huku wakijiwekea akiba iwe msingi mzuri kwa wakati ujao, ili wapate uzima ulio kweli kweli.
Tunaitwa kuwa mawakili wa Mungu;
Mtume Paulo anamwandikia Timotheo kulifundisha Kanisa juu ya kupiga vita vizuri vya imani kwa kuyaepuka mabaya. Katika hilo, moja ya jambo analoandika Paulo ni kutojivunia utajiri, bali katika utajiri huo kumtumaini Mungu. Katika utajiri huo, Paulo anasema watu wafundishwe kuwa wema, wawe tayari kutoa mali zao kwa ajili ya Kristo wakishirikiana na wenzao kwa moyo. Paulo anasisitiza kuweka akiba kwa ajili ya wakati ujao kama msingi wa familia na Kanisa.
Msisitizo wa Paulo asubuhi ya leo ni kutumia mali zetu kwa Utukufu wa Mungu. Mali zetu na vipawa tulivyopewa visitutoe kwa Kristo, bali kutuweka kwake tukitambua kuwa vyote vimetoka kwake na sisi tumewekwa kuwa mawakili wake. Sisi tunafanya kazi kwa ajili ya Bwana, kwa hiyo tutumie mali na vipawa vyetu kwa ajili yake. Tutende mema kwa kushirikiana, kama mawakili wema wa Kristo ili tuwe na mwisho mwema. Amina
Uwe na wiki njema, ukiwa wakili mwema.
Heri Buberwa Nteboya
0784 968650