Date: 
11-09-2025
Reading: 
Zaburi 141:1-5

Alhamisi asubuhi tarehe 11.09.2025

Zaburi 141:1-5

1 Ee Bwana, nimekuita, unijie hima, Uisikie sauti yangu nikuitapo.

2 Sala yangu ipae mbele zako kama uvumba, Kuinuliwa mikono yangu kama dhabihu ya jioni.

3 Ee Bwana, uweke mlinzi kinywani pangu, Mngojezi mlangoni pa midomo yangu.

4 Usiuelekeze moyo wangu kunako jambo baya, Nisiyazoelee matendo yasiyofaa, Pamoja na watu watendao maovu; Wala nisile vyakula vyao vya anasa.

5 Mwenye haki na anipige, itakuwa fadhili; Anikemee, itakuwa kama mafuta kichwani; Kichwa changu kisikatae, Maana siachi kusali kati ya mabaya yao.

Tutumie ndimi zetu kwa Utukufu wa Mungu;

Zaburi ya 141 ni wimbo wa Mfalme Daudi ikiwa sala ya kuomba ukombozi toka majaribu ya shetani, lakini pia kuomba ulinzi dhidi ya maadui wa ndani na nje. Daudi anamuomba Mungu kuuepusha moyo wake na dhambi, na ulimi wake usitoe maneno yasiyo haki. Daudi anaomba asiuelekeze moyo wake kunako jambo baya, na jambo la muhimu anamuomba Bwana awe mlinzi wake. 

Msingi wa sala ya Daudi kama tulivyosoma ni kulindwa dhidi ya uovu. Daudi kwa kutambua kuwa Bwana ndiye Mfalme aliye juu ya vyote, anaomba ulinzi wa Mungu. Daudi anakwenda mbele za Mungu akiomba rehema na ulinzi. Anatumia ulimi wake kwa Utukufu wa Mungu. Tumia ulimi wako kwa utukufu wa Mungu. Amina

Alhamisi njema

 

Heri Buberwa Nteboya 

0784 968650 

bernardina.nyamichwo@gmail.com