Date:
08-01-2025
Reading:
2 Wakorintho 4:6
Hii ni Epifania
Jumatano asubuhi tarehe 08.01.2025
2 Wakorintho 4:6
Kwa kuwa Mungu, aliyesema, Nuru itang'aa toka gizani, ndiye aliyeng'aa mioyoni mwetu, atupe nuru ya elimu ya utukufu wa Mungu katika uso wa Yesu Kristo.
Yesu ni nuru ya Ulimwengu;
Ahadi ya Mungu kwamba nuru itang'aa gizani kama anavyoandika Mtume Paulo ulikuwa ni utabiri wa ujio wa Yesu Kristo, ambaye angekuja kuuokoa ulimwengu. Paulo anaandika kwamba nuru hii iling'aa mioyoni mwetu. Hapa Paulo anamtaja Yesu Kristo ambaye alikuja kuwa nuru kwa wote waaminio.
Ujumbe wa Mtume Paulo asubuhi hii ni mkazo wa Yesu aliyekuja kuuang'azia ulimwengu, yaani kuleta nuru. Kwa maana nyingine, tunakumbushwa kuwa ni Yesu pekee aliyekuja kuleta wokovu kwa Ulimwengu wote. Yeye huwapokea wote wamwaminio, huwatoa gizani wote wampokeao na kuwaingiza nuruni. Mwamini sasa uokolewe. Amina
Jumatano njema
Heri Buberwa