MATANGAZO YA USHARIKA  

TAREHE 15 DECEMBA, 2024

SIKU YA BWANA YA TATU KATIKA MAJILIO (ADVENT)

NENO LINALOTUONGOZA NI TUBUNI NA KUAMINI INJILI

1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli. 

2. Wageni: Hakuna Wageni waliotufikia kwa cheti. 

3. Matoleo ya Tarehe 08/12/2024

Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.

NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:

0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT

Lipa namba M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL

4. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4:30 asubuhi. Vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Morning Glory saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada za mchana saa 7.00 mchana. Alhamisi saa 11.00 jioni tuna kipindi cha Maombi na Maombezi, ambapo tunajifunza neno la Mungu na kupata muda wa kutosha wa maombi. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front TV.

5. Kitenge chetu kipya cha Kiharaka kinapatikana hapo nje na kwenye duka letu la vitabu kwa bei yaTsh. 40,000/=. 

6. Jumapili ijayo tarehe 22/12/2024 katika ibada zote Baraza la Wazee watamshukuru Mungu kwa matendo makuu aliyoyatenda. Wanaomba Washarika wote muwasindikize katika tendo hili kuu la kumshukuru Mungu.

7. Uongozi wa Usharika unapenda kuwataarifu Washarika wenye watoto kuanzia miaka 12 na kuendelea kuandikisha watoto kwa ajili ya darasa la Kipaimara litakaloanza mapema 2025. Fomu zinapatikana ofisi ya Parish Worker.

8. Baba Askofu Dr. Alex Gehazi Malasusa anawaalika Wakristo wote wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani kwenye kusanyiko la fellowship DMP litafanyika leo tarehe 15/12/2024 Usharika wa KKKT Mbezi Beach saa 8.00 mchana. Washarika wote mnakaribishwa.

9. Uongozi wa umoja wa Vijana Azania Front unapenda kuwatangazia vijana wote kuwa kutakuwa na mkutano mkuu wa umoja wa vijana leo jumapili tarehe 15/12/2024 kwanzia saa 3 :30 Asubuhi hadi saa 6:00 mchana, vijana wote mnahimizwa kushiriki .

10. NDOA: NDOA ZA WASHARIKA 

KWA MARA YA KWANZA TUNATANGAZA NDOA YA TAREHE 04/01/2025                    

SAA 9.00 ALASIRI

  • Bw. Blessing Nathaniel Rweikiza na Bi Jesca Philimon Nassari

KWA MARA YA PILI TUNATANGAZA NDOA ZA TAREHE 28/12/2024                    

SAA 7.00 MCHANA

  • Bw. Yusuph Elieza Lazalo na Bi Ainess Solomon Seythiel

NDOA IFUATAYO TAREHE 28/12/2024 KWA MARA YA PILI ITAFUNGWA KKKT SAMANGA KILIMANJARO KATI YA 

  • Bw. Pasque Dudley Mawala na Bi Evelyn Naweaichi Mosha

Matangazo mengine ya Ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo karibu na duka letu la vitabu. 

11. IBADA ZA NYUMBA KWA NYUMBA

  • Mjini kati: Kwa ……………………………………
  • Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo: Kwa Bwana na Bibi Munisi    
  • Kinondoni: Kwa …………………………………………
  • Tegeta, Kunduchi, Bahari Beach, Ununio: Kwa ………………………
  • Mikocheni, Kawe, Mbezi Beach: Kwa ………………………………..
  • Ilala, Chang’ombe, Buguruni: Kwa …………………………………….
  • Oysterbay, Masaki: Kwa …………………………………………………….

12. Zamu: Zamu za wazee ni Kundi la Pili  

Na huu ndiyo mwisho wa matangazo yetu, Bwana ayabariki.