Date:
02-11-2024
Reading:
Zaburi 44:1-5
Jumamosi asubuhi 02.11.2024
Zaburi 44:5-11
[5]Kwa nguvu zako tutawaangusha watesi wetu;
Kwa jina lako tutawakanyaga watupingao.
[6]Maana sitautumainia upinde wangu,
Wala upanga wangu hautaniokoa.
[7]Bali Wewe ndiwe uliyetuokoa na watesi wetu;
Na watuchukiao umewaaibisha.
[8]Tumejisifia Mungu mchana kutwa,
Na jina lako tutalishukuru milele.
[9]Lakini umetutupa, umetufedhehesha,
Wala hutoki na majeshi yetu.
[10]Waturudisha nyuma tukampa mtesi kisogo,
Na watuchukiao wanajipatia mateka.
[11]Umetutoa kama kondoo tuwe chakula,
Na kututawanya kati ya mataifa.
Mwenye haki ataishi kwa imani;
Zaburi tuliyosoma ilikuwa kilio cha kitaifa na sala kwa ajili ya msaada kwa Israeli. Israeli inakiri kuwashinda watesi kwa kumtumaini Mungu, wakimshukuru milele.
Msaada wetu unatoka kwa Yesu Kristo tu, anayetuwezesha kushinda katika njia zetu za kila siku. Hivyo tumpe shukrani zetu, tukimtumaini siku zote.
Siku njema
Heri Buberwa