Date: 
24-10-2024
Reading: 
1 Petro 1:1-6

Alhamisi asubuhi tarehe 24.10.2024

1 Petro 1:6-11

6 Mnafurahi sana wakati huo, ijapokuwa sasa kwa kitambo kidogo, ikiwa ni lazima, mmehuzunishwa kwa majaribu ya namna mbalimbali;

7 ili kwamba kujaribiwa kwa imani yenu, ambayo ina thamani kuu kuliko dhahabu ipoteayo, ijapokuwa hiyo hujaribiwa kwa moto, kuonekane kuwa kwenye sifa na utukufu na heshima, katika kufunuliwa kwake Yesu Kristo.

8 Naye mwampenda, ijapokuwa hamkumwona; ambaye ijapokuwa hamwoni sasa, mnamwamini; na kufurahi sana, kwa furaha isiyoneneka, yenye utukufu,

9 katika kuupokea mwisho wa imani yenu, yaani, wokovu wa roho zenu.

10 Katika habari ya wokovu huo manabii walitafuta-tafuta na kuchunguza-chunguza, ambao walitabiri habari za neema itakayowafikia ninyi.

11 Wakatafuta ni wakati upi, na wakati wa namna gani ulioonywa na Roho wa Kristo aliyekuwa ndani yao, ambaye alitangulia kuyashuhudia mateso yatakayompata Kristo, na utukufu utakaokuwako baada ya hayo.

Tuishindanie Imani katika Kristo Yesu;

Katika somo letu asubuhi hii, Petro anaandika juu ya kuwa na tumaini katika Yesu Kristo. Anaandika kwamba pamoja na kuhuzunishwa na mambo mbalimbali katika safari ya imani, waaminio sharti wavumilie katika Kristo ambaye imani yetu kwake ni zaidi ya dhahabu. Petro anasisitiza kumwamini Yesu aletaye furaha isiyoelezeka, yenye Utukufu.

Petro anatusihi kukaa katika neema ya Mungu, ambayo tumepewa na Yesu Kristo aliyetuokoa kwa kuteswa na kufa msalabani (11). Kwa neema hii tunayo imani ambayo hutufanya kumwamini Yesu katika hali yoyote. Basi tuzingatie kukaa katika Yesu Kristo, tusimuache daima. Amina

Alhamisi njema 

Heri Buberwa