Date: 
26-09-2024
Reading: 
Mithali 3:11-18

Alhamisi asubuhi tarehe 26.09.2024

Mithali 3:11-18

11 Mwanangu, usidharau kuadhibiwa na Bwana, Wala usione ni taabu kurudiwa naye.

12 Kwa kuwa Bwana ampendaye humrudi, Kama vile baba mwanawe ampendezaye.

13 Heri mtu yule aonaye hekima, Na mtu yule apataye ufahamu.

14 Maana biashara yake ni bora kuliko biashara ya fedha, Na faida yake ni nyingi kuliko dhahabu safi.

15 Yeye ana thamani kuliko marijani, Wala vyote uvitamanivyo havilingani naye.

16 Ana wingi wa siku katika mkono wake wa kuume, Utajiri na heshima katika mkono wake wa kushoto.

17 Njia zake ni njia za kupendeza sana, Na mapito yake yote ni amani.

18 Yeye ni mti wa uzima kwao wamshikao sana; Ana heri kila mtu ashikamanaye naye.

Uchaguzi wako ndiyo maisha yako;

Somo la asubuhi ya leo ni maonyo juu ya kumwamini na kumheshimu Mungu. Ni mafundisho juu ya kutodharau kumfuata Bwana. Tunasoma kwamba ni heri yule mwenye hekima na ufahamu, maana maisha yake hujaa mafanikio. Amwaminiye Bwana anao wingi wa siku, utajiri na heshima. 

Tunakumbushwa kumwamini na kumheshimu Mungu ili tuenende katika njia sahihi. Kama tulivyosoma, amwaminiye Bwana hupata mafanikio maana hufuata njia sahihi. Hivyo sisi tunaalikwa kumfuata Yesu na kumwamini, ili tuokolewe na kuurithi uzima wa milele. Amina

Alhamisi njema

Heri Buberwa