Date: 
25-09-2024
Reading: 
Yoshua 24:19-22

Jumatano asubuhi tarehe 25.09.2024

Yoshua 24:19-22

19 Yoshua akawaambia watu, Hamwezi kumtumikia Bwana; kwa kuwa yeye ni Mungu mtakatifu; yeye ni Mungu mwenye wivu; hatawasamehe makosa yenu, wala dhambi zenu.

20 Kama mkimwacha Bwana na kuitumikia miungu migeni, ndipo atageuka na kuwatenda mabaya na kuwaangamiza, baada ya kuwatendea mema.

21 Lakini hao watu wakamwambia Yoshua, La! Lakini tutamtumikia Bwana.

22 Yoshua akawaambia watu, Ninyi mmekuwa mashahidi juu ya nafsi zenu, ya kuwa mmemchagua Bwana, ili kumtumikia yeye. Wakasema, Sisi tu mashahidi.

Uchaguzi wako ndiyo maisha yako;

Yoshua baada ya kuwa amewaongoza wana wa Israeli kuelekea nchi ya ahadi aliwaambia kuwa walitakiwa kumtumikia Mungu wa kweli aliyewakomboa kutoka Misri. Aliwataka kuiacha miungu yao na kuchagua kumtumikia Bwana. Ukisoma kabla unaona Yoshua akiwasisitiza kumtumikia Bwana kwa kuiacha miungu;

Yoshua 24:14-15

14 Basi sasa mcheni Bwana, mkamtumikie kwa unyofu wa moyo na kwa kweli; na kuiweka mbali miungu ambayo baba zenu waliitumikia ng'ambo ya Mto, na huko Misri; mkamtumikie yeye Bwana.
15 Nanyi kama mkiona ni vibaya kumtumikia Bwana, chagueni hivi leo mtakayemtumikia; kwamba ni miungu ile ambayo baba zenu waliitumikia ng'ambo ya Mto, au kwamba ni miungu ya wale Waamori ambao mnakaa katika nchi yao; lakini mimi na nyumba yangu tutamtumikia Bwana.

Ujumbe huu unadumu kwetu hata sasa. Israeli walielekezwa kumtumikia Mungu aliyewatoa utumwani Misri. Sisi tunakumbushwa kumwamini na kumtumikia Bwana aliyetuokoa kwa njia ya kifo cha Yesu msalabani. Huyu ndiye Mwokozi wetu, ambaye yupo nasi daima. Mchague Yesu daima. Amina

Jumatano njema

Heri Buberwa