Date: 
07-09-2024
Reading: 
Mambo ya Walawi 25:35-38

Jumamosi asubuhi tarehe 07.09.2024

Mambo ya Walawi 25:35-38

[35]Na ikiwa ndugu yako amekuwa maskini, na mkono wake umelegea kwako, ndipo utamsaidia, atakaa nawe kama mgeni, na msafiri.

[36]Usitake riba kwake wala faida, bali mche Mungu wako, ili ndugu yako akae nawe.

[37]Usimpe fedha yako upate riba, wala usimpe vyakula vyako kwa kujitakia faida.

[38]Mimi ndimi BWANA, Mungu wako, niliyewatoa katika nchi ya Misri ili niwape nchi ya Kanaani, nipate kuwa Mungu wenu.

Mpende Jirani yako;

Tunasoma kuwa tukimuona mtu maskini tumsaidie haja zake. Tukae naye kama mgeni na msafiri. Mgeni hukirimiwa vizuri, kwa wema na ukarimu. Pia tukimsaidia tusitegemee faida.

Andiko hili linakuja likitukumbusha kusaidia wasiojiweza, kwa vitendo. Sisi kama wakristo tunawajibika kusaidia wasiojiweza, yatima, wazee na wajane. Tunatekeleza hili? Tunajitoa kwa ajili ya utume wa kusaidia wasiojiweza?

Tukifanya hivi tunawapenda hawa ndugu zetu na kuutangaza wema wa Kristo. Tutoe mali zetu kwa ajili ya Bwana kuwasaidia wahitaji, huo ndio upendo kwa jirani, tukizingatia kuwa mali zote tumepewa na Mungu. Amina

Jumamosi njema.

Heri Buberwa