Date: 
29-05-2024
Reading: 
1Wakorintho 3:1-9

Jumatano asubuhi tarehe 29.05.2024

1 Wakorintho 3:1-9

1 Lakini, ndugu zangu, mimi sikuweza kusema nanyi kama na watu wenye tabia ya rohoni, bali kama na watu wenye tabia ya mwilini, kama na watoto wachanga katika Kristo.

2 Naliwanywesha maziwa sikuwalisha chakula; kwa kuwa mlikuwa hamjakiweza. Naam, hata sasa hamkiwezi,

3 kwa maana hata sasa ninyi ni watu wa tabia ya mwilini. Maana, ikiwa kwenu kuna husuda na fitina, je! Si watu wa tabia ya mwilini ninyi; tena mnaenenda kwa jinsi ya kibinadamu?

4 Maana hapo mtu mmoja asemapo, Mimi ni wa Paulo; na mwingine, Mimi ni wa Apolo, je! Ninyi si wanadamu?

5 Basi Apolo ni nani? Na Paulo ni nani? Ni wahudumu ambao kwao mliamini; na kila mtu kama Bwana alivyompa.

6 Mimi nilipanda, Apolo akatia maji; bali mwenye kukuza ni Mungu.

7 Hivyo, apandaye si kitu, wala atiaye maji, bali Mungu akuzaye.

8 Basi yeye apandaye, na yeye atiaye maji ni wamoja, lakini kila mtu atapata thawabu yake mwenyewe sawasawa na taabu yake mwenyewe.

9 Maana sisi tu wafanya kazi pamoja na Mungu; ninyi ni shamba la Mungu, ni jengo la Mungu.

Utatu Mtakatifu; Iweni na nia ya Kristo;

Mtume Paulo alikuwa anawaambia Wakorintho juu ya ubinafsi, yaani kujiona bora katika Ufalme wa Mungu kwa sababu unamfuata fulani. Katika sura ya tatu anawaambia kuwa hiyo ni tabia ya mwilini. Hatua yake ya awali ya kuwaambia kuwa wamoja katika Kristo anaiita "kuwanywesha maziwa", kwamba alikuwa anawaambia ipasavyo kuamini katika Bwana mmoja, Yesu Kristo aliye Mwokozi wa ulimwengu.

Paulo anasema apandaye na atiaye maji, wote ni wamoja. Wote hawa hufanya kazi pamoja katika Bwana. Ujumbe kwetu asubuhi hii ni kila mmoja wetu kuamini katika Kristo tukikaa pamoja kwa umoja. Tukitumika pamoja shambani mwa Bwana kwa karama zetu, tutawavuta wengi kwa Yesu. Tushirikiane ili tuimarike. Amina

Jumatano njema 

Heri Buberwa