Date: 
17-07-2023
Reading: 
Tito 3:4+

Jumatatu asubuhi tarehe 17.07.2023

Tito 3:4

4 Lakini wema wake Mwokozi wetu Mungu, na upendo wake kwa wanadamu, ulipofunuliwa, alituokoa;

Amri ya upendo.

Mtume Paulo anaianza sura ya tatu kwa Tito kwa kumwambia kuwa awafundishe watu kuwa wanyenyekevu, watiifu, wasiotukana, wasio wagomvi, wema na wenye upole kwa watu wote. Anamtuma kufundisha watu kuachana na historia ya kutenda uovu;

Tito 3:3

Maana hapo zamani sisi nasi tulikuwa hatuna akili, tulikuwa waasi, tumedanganywa, huku tukitumikia tamaa na anasa za namna nyingi, tukiishi katika uovu na husuda, tukichukiza na kuchukiana.

Sasa hadi hapo tunaona Paulo akimtuma Tito kufundisha juu ya kuacha uovu, na kuishi kwa upendo. 

Katika mstari wa 4 Paulo anasema wema wa Mungu na upendo wake ulipofunuliwa ulituokoa, ndiyo maana katika upendo huo Paulo anasisitiza Kanisa kutenda mema.

Kama vile Kristo alivyotuokoa kwa wema na neema yake, anatuita kupendana sisi sote, kama kundi la waaminio. Haimaanishi tusiwapende wasioamini, bali tupendane kama Taifa la Mungu tukishuhudia habari za Kristo aokoaye. Tuishi tukitenda mema, upendo ukiwa kati yetu.

Uwe na wiki njema yenye ushuhuda. Amina.

 

Heri Buberwa