Hii ni Kwaresma
Alhamisi asubuhi 09.03.2023
Mathayo 27:3-10
3 Kisha Yuda, yule mwenye kumsaliti, alipoona ya kuwa amekwisha kuhukumiwa, alijuta, akawarudishia wakuu wa makuhani na wazee vile vipande thelathini vya fedha, akasema, Nalikosa nilipoisaliti damu isiyo na hatia.
4 Wakasema, Basi, haya yatupasani sisi? Yaangalie haya wewe mwenyewe.
5 Akavitupa vile vipande vya fedha katika hekalu, akaondoka; akaenda, akajinyonga.
6 Wakuu wa makuhani wakavitwaa vile vipande vya fedha, wakasema, Si halali kuviweka katika sanduku ya sadaka, kwa kuwa ni kima cha damu.
7 Wakafanya shauri, wakavitumia kwa kununua konde la mfinyanzi liwe mahali pa kuzika wageni.
8 Kwa hiyo konde lile huitwa konde la damu hata leo.
9 Ndipo likatimia neno lililonenwa na nabii Yeremia, akisema, Wakavitwaa vipande thelathini vya fedha, kima chake aliyetiwa kima, ambaye baadhi ya Waisraeli walimtia kima;
10 wakavitumia kwa kununua konde la mfinyanzi, kama Bwana alivyoniagiza.
Ukatili ni uovu;
Baada ya Yesu kukamatwa, ni asubuhi ambapo wakuu wa makuhani ma wazee wanakata shauri la kumwua. Yesu anapelekwa kwa Pilato, na Yuda aliyemsaliti anajinyonga. Yuda alivirudisha vipande vya fedha alivyopewa, wale makuhani hawakuvitunza hekaluni bali kununua konde la mfinyanzi. Wakati yote haya yakiendelea Yesu anapelekwa kwa Pilato.
Ni njia ya mateso ambayo haikuwa rahisi. Ilihusisha mateso yaliyojaa kipigo kikali na dharau kubwa. Lakini Yesu alikinywea kikombe kile! Ni upendo wake kwetu uliomtuma kufanya vile, yaani kufa kwa ajili ya dhambi za ulimwengu, ili ulimwengu uokolewe katika yeye. Tuishi maisha ya toba mbele za Mungu ili tuwe na mwisho mwema. Siku njema.
Heri Buberwa