MATANGAZO YA USHARIKA
TAREHE 19 MACHI, 2023
NENO LINALOTUONGOZA SIKU YA LEO NI
YESU NI CHAKULA CHA UZIMA
1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.
2. Wageni: Hakuna mgeni aliyetufikia kwa cheti.
3. Matoleo ya Tarehe 12/03/2023
Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wakumtolea
kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.
NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:
- 0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT
- Namba ya Wakala M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT
CATHEDRAL
4. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za
jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza
saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza
saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa
4:30 asubuhi. vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku
za juma. Morning Glory saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa
Mungu, Ibada za mchana saa 7.00 -7.30 mchana tunapopata faragha binafsi
na Mungu. Alhamisi jioni saa 11.00 jioni tuna kipindi cha Maombi na
Maombezi, ambapo tunajifunza neno la Mungu na kupata muda wa kutosha
wa maombi. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front TV.
Karibu.
5. Ratiba yetu ya mafundisho katika msimu wa Kwaresma hapa Kanisa Kuu,
inaendelea. Na kwa wiki hii ya tarehe 12 hadi 18 Machi tutakuwa na
A. Ibada ya Majivu siku ya Jumatano, na
B. Semina ya Neno la Mungu kuanzia hiyo J5 tarehe 22 hadi Ijumaa tarehe 24
Machi 2023.
Semina zetu za Kwaresma zitaendelea kama zilivyopangwa hadi mwisho wa
msimu tarehe 31 Machi 2023. Vipindi vyote vinaanza saa 11:00 jioni. Karibuni
wote tumfanyie Mungu Ibada njema.
6. Leo tarehe 19/03/2023 mara baada ya ibada tutakuwa na Mkutano Mkuu wa
Usharika.
7. Uongozi wa Umoja wa Wanawake unapenda kuwakumbusha wale wote
waliochukua kadi za kuchangia ada za watoto Yatima ambao bado
hawajarudisha au kukamilisha ahadi zao waweze kukamilisha ifikapo tarehe
31 Machi 2023. Tunatanguliza shukrani kwa sadaka zenu kwa ajili ya watoto
hao. Mungu awabariki.
8. Jumamosi ya Tarehe 01/04/2023 saa 3.00 asubuhi kutakuwa na ibada ya
wazee kuanzia miaka 60. Washarika tuendelee kuiombea siku hiyo.
9. Jumamosi ijayo tarehe 25/03/2023 saa 3.00 asubuhi mpaka saa 7.00 mchana
hapa usharikani Azania Front Cathedral kutakuwa na Semina ya Wajane na
Wagane. Mnenaji atakuwa ni Mama Hevenlight Swai kutoka usharika wa
Kariakoo. Wote mnakaribishwa.
10. Jumapili ijayo tarehe 26/03/2023 tutashiriki Chakula cha Bwana. Washarika
Tujiandae.
11. IBADA ZA NYUMBA KWA NYUMBA
- Oysterbay na Masaki:/ Mikocheni, Kawe, Mbezi Beach Watashiriki
ibada hapa Usharikani
- Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo:
Kwa Mama Ruth Korosso
- Mjini kati: Hapa Usharikani Jumamosi saa 1.00 asubuhi
- Ilala, Chang’ombe na Buguruni: Kwa Dada Christina
- Kinondoni: Kwa Mama Hilda Lwezaula
- Tegeta, Kunduchi, Bahari Beach, Ununio: Kwa …………..
- Upanga: Kwa Bwana na Bibi George Kinyaha Alykhan road
- Tabata: Kwa Mch. Aston Kibona
12. MAHUDHURIO YA IBADA - TAREHE 12/03/2023
Jumla ibada zote watu ….. 710
13. Zamu: Zamu za wazee ni Wazee wote watakuwa zamu
Na huu ndiyo mwisho wa matangazo yetu, Bwana ayabariki.