MATANGAZO YA USHARIKA

TAREHE 03 FEBRUARI, 2019

SIKU YA BWANA YA 4 KATIKA MAJIRA YA UFUNUO

NENO LINALOTUONGOZA SIKU YA LEO NI

MUNGU ANATULINDA

 

1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.

2. Wageni: Hakuna Mgeni aliyefika na cheti. 

3. Alhamisi ijayo tarehe 07/02/2019 saa 11.30 jioni tutakuwa na kipindi cha Maombi na Maombezi. Karibuni tuendelee kujikabidhi kwa Mungu, ili kuhakikisha tunatembea na Mungu katika mwaka huu, akitia nuru mioyoni mwetu ili tujue tumaini tulilowekewa mwaka huu pia.  Wote mnakaribishwa.

4. Umoja wa Wanaume Azania Front unayo furaha kuwatangazia kuwa kutakuwa na semina ya siku moja hapa Usharikani tarehe 16/02/2019 saa 4.00 mpaka saa 6 mchana.  Mnenaji atakuwa ni Mch. Dr. Kimilike kutoka Njombe. Mada Kuu:  Biblia na Uchumi. Jiandae kupokea Baraka hizo.

5. Leo tarehe 03/02/2019 ni siku yetu maalum ya kumtolea Mungu sadaka yetu ya Zaka, yaani fungu la kumi la mapato yetu binafsi na ya mradi na kampuni zetu.  Sadaka hii itaandamana na maombi na maombezi juu ya ufanisi na afya na Maendeleo yetu, familia na vitega Uchumi vyetu.

6. Shukrani:

Jumapili ijayo tarehe 10/02/2019 Katika ibada ya pili

7. Kwaya Kuu ya Usharika itamtolea Mungu shukrani kwa kuwapa afya njema kumaliza mwaka 2018 salama na kuiingia mwaka Mpya 2019.

Neno:  Zaburi 121, Wimbo: Nitayainua macho yangu (Kwaya Kuu)

8. Familia ya Mama Muloelye Mkoma watamshukuru Mungu kwa Mama Muloelye Mkoma kutimiza miaka 80 tarehe 10/2/2019.

Neno:  2 Wakoritho 4:16, Wimbo: TMW 262

9. Jumapili ijayo tarehe 10/02/2019 ni siku ya ubatizo wa watoto na kurudi kundini.  Watakaohitaji huduma hii wafike ofisi ya Mchungaji.

10. Tunapenda kuwakaribisha washarika wote kwenye Mkutano wa injili ulioandaliwa na Uongozi wa KKKKT Dayosisi ya Mashariki na Pwani, utakaoanza tarehe 10 hadi 24 Februari katika viwanja vya iliyokuwa TanganyikaPacker’s Kawe.  Mkutano utaanza kila siku saa 10.00 jioni.  Hivyo basi, ratiba za matukio usharikani kwa kipindi hicho chote, utabadilika. Wote tunaombwa kuuombea mafanikio mkutano huo na kuhudhuria.

11. NDOA – Hakuna Ndoa za Washarika.

Matagazo mengine ya Ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa matagazo karibu na duka letu la vitabu.

12. Ibada za Nyumba kwa Nyumba

      - Mwenge,Kijitonyama, Makumbusho, Sinza, Ubungo na Makongo: Kwa Bi Mary Kinisa

      - Mjini kati: Kwa Mama  Victoria Mwansasu

      - Ilala/Chag’ombe/Mivinjeni: Kwa Bwana na Bibi Kowero

     - Kawe/Mikocheni/Mbezi Beach: Kwa Bibi Erica Byabato

     - Tabata: Kwa Bwana na Bibi Mwakasege

     - Upanga: Kwa Bwana na Bibi Munisi

     - Kinondoni: Kwa Bwana na Bibi Edward Mkony