MATANGAZO YA USHARIKA
TAREHE 08 JULAI, 2018
SOMO LINALOTUONGOZA SIKU YA LEO NI 'UPENDO WA MUNGU NA UTAWALE'
1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.
2. Wageni: Wageni waliotufikia na cheti ni Simon Tweve – toka kanisala Anglikana - Kongowe
3. Tunamshukuru Mungu kwa jinsi anavyojidhihirisha kila tunapokutana kwa masomo, maombi na maombezi. Hivyo kuanzia jumatatu tarehe 09/07/2018 hadi ijumaa tarehe 13/07/2018 tutaendelea na kipindi cha Morning Glory kikiongozwa na Mwl. Mgisa Mtebe. Aidha siku ya alhamisi tarehe 12/07/2018 kuanzia saa 11.30 jioni tutakuwa na kipindi cha maombi na maombezi. Washarika wote mnakaribishwa.
4. Leo ni sikukuu ya Umoja wa Vijana hivyo ibada zote zitaongozwa na vijana.
5. Jumamosi ijayo tarehe 14/-7/2018 ni siku ya tamasha la uimbaji wa kwaya ya Wanawake. Tamasha hili litafanyika Usharika wa Kitunda Relini. Hivyo wiki hii kutakuwa na mazoezi siku ya Jumatano, Alhamisi na Ijumaa. Wanawake wote wanaombwa kushirikiana pamoja katika kumsifu Mungu.
6. Jumapili ijayo tarehe 15/07/2018 katika ibada ya pili familia ya Marehemu Theogoni Amrini pamoja na kwaya ya Vijana watamshukuru Mungu kwa matendo makuu aliyowatendea ikiwa ni pamoja na kuwafanikisha kumaliza msiba salama.
7. Neno: Zaburi 103:1-22, Wimbo: Kwaya ya Vijana
8. NDOA.
NDOA ZA WASHARIKA
KWA MARA YA PILI TUNATANGAZA NDOA ZA TAREHE 21/07/2018 SAA 08.00 MCHANA
Bw. Mika Mathayo Ndosa na Bi Marystela Kondo Benedict
SAA 09.00 ALASIRI
Bw. Amani Goodluck Kamnde na Bi Anna Cecilia Katarina Westman
Matangazo mengine ya ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo Karibu na duka letu la vitabu
9. Ibada za Nyumba kwa Nyumba
Kinondoni: Kwa Mama Hilda Lwezaula
Mjini kati: Kwa Mama Omega Mongi
Kijitonyama/Sinza/Mwenge/Makumbusho/Ubungo: Kwa Bwana na Bibi Charles Lyimo
Wazo/tegeta/Kunduchi/BahariBeach/Ununio: Kwa Bwana na Bibi David Korosso
Zamu: Zamu za wazee ni kundi la Pili watashirikiana na Vijana.
Na huu ndio mwisho wa matangazo yetu, Mungu ayabariki.