MATANGAZO YA USHARIKA
TAREHE 27 AGOSTI, 2017
NENO LINALOTUONGOZA SIKU YA LEO NI MUNGU HUWAPINGA WENYE KIBURI, BALI HUWAINUA WANYENYEKEVU
1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.
2. Wageni: wageni waliotufikia na cheti ni Dr. Janet Mwambona toka Gaborone Congregation Lutheran Church Botswana. Anahamia hapa.
3. Leo hatutakuwa na kipindi cha Maombi na Maombezi hapa Usharikani ili kuwapa nafasi Wanawake kuhudhuria semina inayoongozwa na Mwl. Christopher Mwakasege Viwanja vya Tanganyika Packers Kawe, ila huduma itaendelea siku ya Alhamisi 31/08/2017 Kipindi kitaongozwa na Mwinjilisti Emmanuel Frank wa KKKT Tumbi.Wote mnakaribishwa.
4. Vitenge vya Kiharaka bado vipo, vitauzwa hapo nje kwa bei ya shilingi elf 10.Kama umeshanunua unaweza kumnunulia ndugu, rafiki ili tuweze kufanikisha ujenzi wa kituo chetu cha Kiroho Kiharaka.
5. Mkutano wa VICOBA ya Wajane na Wagane wa Azania Front utafanyika siku ya Jumamosi tarehe 02/09/2017 kuanzia saa 3.00 asubuhi. Wahusika wote wanaombwa kuhudhuria.
6. Leo tutashiriki Chakula cha Bwana. Washarika karibuni.
7. Jumapili ijayo tarehe 03/09/2017 tutamtolea Mungu Fungu la kumi.Washarika tujiandae.
8. Kamati ya Afya na Ustawi wa Jamii Azania Front inapenda kuwatangaziawasharika wote kuwa mafundisho ya Elimu ya Afya kwa wanafunzi wa Kipaimara kwa mwaka huu yatafanyika tarehe 23 Septemba 2017 kuanzia saa 3.00 asubuhi hadi saa 8.00 mchana.Mafundisho haya yatawajumuisha pia wazazi wa watoto hawa na vile vile waliopata Kipaimara kwa miaka ya hivi karibuni na walio na umri hadi miaka 15.Tunaomba wanafunzi na wazazi watakaoshiriki mafundisho hayo wajiandikishe kwa Parish Worker au kwa Katibu wa Kamati ya Afya na Ustawi wa Jamii Dr. Lillian Mbowe.
9. Morogoro Lutheran Junior seminary inakaribisha maombi ya kujiunga na kidato cha kwanza kwa mwaka 2018.Barua za maombi zipelekwe ofisi kuu ya Dayosisi mapokezi, Luther House, ghorofa ya kwanza. Kila mwombaji atatakiwa kulipa ada ya Tshs. 15,000/=. Barua ya maombi iwe fupi ikieleza ombi la kujiunga kidato cha kwanza, jina la mtoto, umri wake, shule ya msingi aliyosoma, usharika/Mtaa wanaoabudu wazazi, pia atafanya mtihani kwa lugha ya Kiswahili au Kiingereza (English Medium) pia weka namba za simu. Mwisho wa maombi ni Tarehe 08/09/2017. Maelezo zaidi yamebandikwa kwenye ubao wa Matangazo Karibu na duka letu la vitabu.
10. NDOA ZA WASHARIKA
KWA MARA YA PILI TUNATANGAZA NDOA ZA TAREHE 10/09/2017
SAA 08.00 MCHANA
Bw. Samson Felix mkwama na Bi. Naomi Joel Kiangi
Matangazo mengine ya Ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo Karibu na duka letu la vitabu.
11. Ibada za Nyumba kwa Nyumba
- Upanga: Watatangaziana
- Kinondoni: Kwa Bwana na Bibi Saitiel Kulaba
- Kawe/Mikocheni/Mbezi Beach: Kwa Mama Victoria Mandari
- Tabata: Watatangaziana
- Kijitonyama/Sinza/Mwenge/Makumbusho/Ubungo: Kwa Bwana na Bibi Makwe
- Mjini kati: Kwa Bwana na Bibi Stanley Mkocha
- Wazo/tegeta/Kunduchi/BahariBeach/Ununio:Kwa Bwana na Bibi Buchanagandi
Zamu: Zamu za wazee leo ni kundi la Kwanza
Na huu ndio mwisho wa matangazo yetu, Mungu ayabariki.