MATANGAZO YA USHARIKA

TAREHE 20 NOVEMBA, 2016

NENO LINALOTUONGOZA SIKU YA LEO NI UZIMA WA ULIMWENGU UJAO

 1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.
 1. Uongozi wa Umoja wa Wanawake unapenda kuwatangazia kuwa tarehe 3.12.2016 ni siku ya maadhimisho ya Krismas Kijimbo. Maadhimisho hayo yatafanyika Usharika wa Kariakoo na tarehe 10.12.2016 itakuwa ni maadhimisho ya Krismas Kidayosisi yatakayofanyika Usharika wa Mkuza kuanzia saa 2.00 asubuhi. Wanakwaya wa vikundi vyote mnaombwa kuungana na Kwaya ya wanawake. Mazoezi ni jumatano saa 10.00 jioni.
 1. Kamati ya Misioni na Uinjilisti inapenda kumshukuru Mungu sana kwa jinsi alivyowezesha kuwepo na mafanikio makubwa katika kipindi kifupi katika ibada za maombi na maombezi zinazofanyika hapa usharikani kila siku ya jumapili saa 9.00 alasiri  na siku ya alhamisi saa 11.00 jioni.  Kweli tumemwona Mungu.
 1. Bibi Violet Maro atamshukuru mungu jumapili ijayo tarehe 27.11.2016 katika ibada ya pili kwa Mambo mengi aliyomtendea na familia yake ikiwa ni pamoja na kutimiza umri wa miaka 80.

 Neno: Zab. 5:1-4,  Wimbo: Bwana Mungu nashangaa (391)

 1. NDOA:

NDOA ZA WASHARIKA

KWA MARA YA PILI TUNATANGAZA NDOA ZA TAREHE 03.12.2016

SAA 8.00 MCHANA

Bw. Elifasi Godfrey mrita           na     Bi. Sarah Isidore Temba

      Matangazo mengine ya Ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo karibu na duka letu la vitabu

 1. Ibada za Nyumba kwa Nyumba
 • Upanga: Kwa Bwana na Bibi William Sabaya
 • Kinondoni: Kwa Prof na Bibi Kulaba
 • Ilala/Chang’ombe/Mivinjeni: kwa Dk na Bibi Ruhago
 • Kawe/Mikocheni/Mbezi Beach: Kwa Bwana na Bibi Robson Monyo
 • Oysterbay/Masaki: Kwa mama Mercy Mengi
 • Tabata: Watatangaziana
 • Kijitonyama/Sinza/Mwenge/Makumbusho/Ubungo: Kwa Bwana na Bibi Sangiwa
 • Mjini kati: Watatangaziana
 • Wazo/tegeta/Kunduchi/BahariBeach/Ununio:  Kwa Bwana na Bibi Simbeye

 

Zamu: Zamu za wazee ni kundi la Pili

Na huu ndio mwisho wa matangazo yetu, Mungu ayabariki  

 

MZEE ZEBADIA MOSHI                -        NENO LA WARAKA   - Yn. 14:1-6                                                                                           NENO LA PILI         -  Uf. 21:1-5

MZEE ELIBARIKI MOSHI               -        MATANGAZO