MATANGAZO YA USHARIKA
TAREHE 20 MEI, 2018
SOMO LINALOTUONGOZA SIKU YA LEO ROHO MTAKATIFU HUTUWEZESHA
1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.
2. Wageni: Hakuna wageni waliotufikia na cheti:
3. Alhamisi ijayo tarehe 24/05/2018 kutakuwa na kipindi cha maombi na maombezi yatakayoanza saa 11.30 jioni. Mwalimu atakuwa Mwinjilist Baraka Mbise kutoka KKKT Ubungo, ambaye pia atahudumu Morning Glory kwa wiki nzima kuanzia jumatatu tarehe 21/05/2018. Washarika wote mnakaribishwa.
4. Idara ya Theolojia, Misioni na Uinjilisti Dayosisi ya Mashariki na Pwani inapenda kuwajulisha vijana wote kuwa, kutakuwa na kongamano la vijana KKKT Taifa litakalowakutanisha vijana 1000 kutoka katika Dayosisi zote za KKKT. Kongamano hili litafanyika tarehe 20-25/06/2018 KASSA CHARITY SCHOOL, MWANZA. Gharama za ushiriki kwa kila kijana ni Tshs. 250,000/=. Fomu ya kuchangia kongamano hili la vijana zimeshagawiwa kwa vijana. Aidha kutakuwa na Kongamano la vijana Jimbo la kati litakalofanyika tarehe 03-08/07/2018 katika shule ya Kanisa Peace House Secondary – Arusha. Gharama kwa kila kila kijana mshiriki ni Tsh. 180,000/=. Vijana wote mnaombwa kushiriki, ni muhimu sana.
5. Jumatatu ijayo yaani kesho tarehe 21/05/2018 saa 11.00 jioni kutakuwa na ibada ya Pentekoste. Kwaya zote zitahudumu. Zamu za wazee itakuwa ni kundi la Kwanza.
6. Jumapili ijayo tarehe 27/05/2018 tutashiriki chakula cha Bwana. Hivyo kama kawaida ibada ya pili itaanza saa 4.00 asubuhi. Washarika tujiandae.
7. Uongozi wa wanawake Dayosisi umemeandaa mkesha wa Wanawake wote wa Dayosisi utakaofanyika Ijumaa ijayo tarehe 25/05/2018 Usharika wa Kijitonyama kuanzia saa 3.00 usiku. Wanawake wote mnaombwa kuhudhuria mkesha huu muhimu sana.
8. Mazoezi ya Reformation kwa mwaka 2018 ya naanza mapema siku ya Jumanne tarehe 22/05/2018 saa 11.00 jioni. Kwaya ya Umoja na wale wanaopenda kuimba wanakaribishwa kwa ajili ya mazoezi.
9. Mkutano wa VICOBA ya Wajane na Wagane ya Azania Front utafanyika siku ya jumamosi tarehe 02/06/2018 saa 3.00 asubuhi. Wahusika wote wanaombwa kuhudhuria Mkutano huu.
10. NDOA.
NDOA YA WASHARIKA
KWA MARA YA TATU TUNATANGAZA NDOA ZA TAREHE 26/05/2018
SAA 8.00 MCHANA
Bw. Sepi Lionel Mawalla na Bi. Jestina Joseph Ngowi
Matangazo mengine ya ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo Karibu na duka letu la vitabu.
11. Ibada za Nyumba kwa Nyumba
- Upanga: KwaBwana na Bibi Kavugha
- Kinondoni: Kwa Bwana na., Bibi Alpha Mlenga
- Ilala/Chang’ombe/Mivinjeni: Kwa Mama Doscar Vuhahula
- Kawe/Mikocheni/Mbezi Beach: Kwa Mzee Arnold Kilewo
- Mjini kati: Kwa Bwana na Bibi Stanley Mkocha
- Kijitonyama/Sinza/Mwenge/Makumbusho/Ubungo: Kwa Mama Mamkwe
- Wazo/tegeta/Kunduchi/BahariBeach/Ununio: Kwa Eng. na Bibi Mcharo Mlaki
- Tabata: Kwa Mchungaji Aston Kibona
Zamu: Zamu za wazee ni kundi la Kwanza.
Na huu ndio mwisho wa matangazo yetu, Mungu ayabariki.