Date: 
26-02-2022
Reading: 
Ezekiel 18:20-22

Jumamosi asubuhi tarehe 26.02.2022

Ezekieli 18:20-22

20 Roho itendayo dhambi, ndiyo itakayokufa; mwana hatauchukua uovu wa baba yake, wala baba hatauchukua uovu wa mwanawe, haki yake mwenye haki itakuwa juu yake, na uovu wake mwenye uovu utakuwa juu yake.

21 Lakini mtu mbaya akighairi, na kuacha dhambi zake zote alizozitenda, na kuzishika amri zangu zote, na kutenda yaliyo halali na haki, hakika ataishi, hatakufa.

22 Dhambi zake zote alizozitenda hazitakumbukwa juu yake hata mojawapo; katika haki yake aliyoitenda ataishi.

Neno la Mungu lina nguvu;

Nabii Ezekieli anatoa ujumbe wa uwajibikaji kwa kila mmoja wetu. Anaposema mwana hatauchukua uovu wa baba yake, na baba hatauchukua uovu wa mwanae, anamaanisha kila mmoja wetu kuwajibika kwa nafasi yake katika kumfuata Mungu. 

Yesu anatuita kuacha dhambi. Yaani anatuita kuishi maisha ya toba mbele za Mungu. Anatuita kughairi na kuyaacha maisha ya dhambi ili tuwe wenye haki, ambapo anaahidi kutozikumbuka dhambi zetu. Tutayaacha maisha ya dhambi tukilishika neno lake.

Siku njema.