Date: 
29-04-2019
Reading: 
Exodus 4:10-17 (Kutoka 4:10-17)

MONDAY 29TH APRIL 2019 MORNING                                                 

Exodus 4:10-17 New International Version (NIV)

10 Moses said to the Lord, “Pardon your servant, Lord. I have never been eloquent, neither in the past nor since you have spoken to your servant. I am slow of speech and tongue.”

11 The Lord said to him, “Who gave human beings their mouths? Who makes them deaf or mute? Who gives them sight or makes them blind? Is it not I, the Lord? 12 Now go; I will help you speak and will teach you what to say.”

13 But Moses said, “Pardon your servant, Lord. Please send someone else.”

14 Then the Lord’s anger burned against Moses and he said, “What about your brother, Aaron the Levite? I know he can speak well. He is already on his way to meet you, and he will be glad to see you. 15 You shall speak to him and put words in his mouth; I will help both of you speak and will teach you what to do. 16 He will speak to the people for you, and it will be as if he were your mouth and as if you were God to him. 17 But take this staff in your hand so you can perform the signs with it.”

When God called Moses to lead His people Moses felt inadequate for the task. Moses said he was not able to speak. But God helped Him and Moses became effective in the task to which God called him.

What is God calling you to do? Are you willing? Listen to God’s call every day. Be willing to obey Him. Be available and God will enable you and use you.   

JUMATATU TAREHE 29 APRILI 2019 MORNING                                

KUTOKA 4:10-17

10 Musa akamwambia Bwana Ee Bwana, mimi si msemaji, tokea zamani, wala tokea hapo uliposema na mtumishi wako; maana mimi si mwepesi wa kusema, na ulimi wangu ni mzito. 
11 Bwana akamwambia, Ni nani aliyekifanya kinywa cha mwanadamu? Au ni nani afanyaye mtu kuwa bubu au kiziwi, au mwenye kuona, au kuwa kipofu? Si mimi, Bwana? 
12 Basi sasa, enenda, nami nitakuwa pamoja na kinywa chako, na kukufundisha utakalolinena. 
13 Akasema, Ee Bwana, nakuomba, tuma kwa mkono wake huyo utakayemtuma. 
14 Hasira ya Bwana ikawaka juu ya Musa, akasema, Je! Hayuko Haruni, ndugu yako, Mlawi? Najua ya kuwa yeye aweza kusema vizuri. Pamoja na hayo, tazama, anakuja kukulaki; naye atakapokuona, atafurahi moyoni mwake. 
15 Nawe utasema naye, na kuyatia maneno kinywani mwake; nami nitakuwa pamoja na kinywa chako, na pamoja na kinywa chake, na kuwafundisheni mtakayofanya. 
16 Naye atakuwa msemaji wako kwa watu, hata yeye atakuwa mfano wa kinywa kwako, nawe utakuwa mfano wa Mungu kwake. 
17 Nawe utatwaa fimbo hii mkononi mwako, na kwa hiyo utazifanya zile ishara. 

Wakati Mungu alipomwita Musa, alijisikia kwamba hawezi. Musa alisema kwamba yeye si msemaji. Lakini Mungu alimsaidia na aliwezeshwa kuwa mtumishi shujaa.

Mungu anakuita wewe pia. Mungu ana kazi ya wewe kufanya. Ukimtii atakuwezesha. Usiogope. Kubali na Mungu atakubariki na kukutumia kuwa baraka kwa watu wengine.