WENESDAY 27/06/2018
Esther 4:12-17 New International Version (NIV)
12 When Esther’s words were reported to Mordecai, 13 he sent back this answer: “Do not think that because you are in the king’s house you alone of all the Jews will escape. 14 For if you remain silent at this time, relief and deliverance for the Jews will arise from another place, but you and your father’s family will perish. And who knows but that you have come to your royal position for such a time as this?”
15 Then Esther sent this reply to Mordecai: 16 “Go, gather together all the Jews who are in Susa, and fast for me. Do not eat or drink for three days, night or day. I and my attendants will fast as you do. When this is done, I will go to the king, even though it is against the law. And if I perish, I perish.”
17 So Mordecai went away and carried out all of Esther’s instructions.
In the above verses we see how Esther and her people used prayer to God to intercede in their life threatening problem with the ruling king at that time. We too should use prayer to for God to intercede in our problems. Own our own the mountains we face may seem insurmountable. But with God all is possible.
JUMATANO TAREHE 27/06/2018
ESTA 4:12-17
12 Basi wakamwambia Mordekai maneno ya Esta.
13 Naye Mordekai akawaagiza wampelekee Esta jibu la kusema, Wewe usijidhanie kuwa wewe utaokoka nyumbani mwa mfalme, zaidi ya Wayahudi wote.
14 Kwa maana wewe ukinyamaza kabisa wakati huu, ndipo kutakapowatokea Wayahudi msaada na wokovu kwa njia nyingine; ila wewe utaangamia pamoja na mlango wote wa baba yako; walakini ni nani ajuaye kama wewe hukuujia ufalme kwa ajili ya wakati kama huo?
15 Basi Esta akawatuma ili wamjibu Mordekai,
16 Uende ukawakusanye Wayahudi wote waliopo hapa Shushani, mkafunge kwa ajili yangu; msile wala kunywa muda wa siku tatu, usiku wala mchana, nami na wajakazi wangu tutafunga vile vile; kisha nitaingia kwa mfalme, kinyume cha sheria; nami nikiangamia, na niangamie.
17 Basi Mordekai akaenda zake, akafanya yote kama vile Esta alivyomwagiza.
Katika mistari hapo juu tunaona jinsi Esta na watu wake walivyotumia maombi kwa Mungu kuombea awaponye na shida ya mfalme aliyetaka kuwaangamiza. Sisi pia tunapaswa kutumia maombi kwa ajili ya Mungu kuingilia kati katika matatizo yetu. Milima tunayokabiliana nayo inaweza kuonekana kuwa mikubwa ya kutisha. Lakini kwa Mungu yote yanawezekana.