Date: 
04-04-2022
Reading: 
Zaburi 2:1-4

Hii ni Kwaresma 

Jumatatu asubuhi tarehe 04.04.2022

Zaburi 2:1-4

1 Mbona mataifa wanafanya ghasia, Na makabila wanatafakari ubatili?

2 Wafalme wa dunia wanajipanga, Na wakuu wanafanya shauri pamoja, Juu ya Bwana, Na juu ya masihi wake.

3 Na tuvipasue vifungo vyao, Na kuzitupia mbali nasi kamba zao.

4 Yeye aketiye mbinguni anacheka, Bwana anawafanyia dhihaka.

Yesu Kuhani Mkuu;

Asubuhi hii tunasoma wimbo unaowashangaa watu wafanyao ghasia na kufanya ubatili. Yaani ni watu wanaotumia muda wao kufanya yasiyofaa, na tafakari zisizo na utukufu wa Mungu. Tunawasoma wafalme na viongozi wengine wanaokwenda kinyume na mapenzi ya Mungu, Bwana akiwashangaa!

Katika majira haya ya mateso, nini tunatafakari juu ya Yesu Kristo? Ni wakati wa kumtafakari kama Mwokozi wa ulimwengu, aliye juu ya vyote. Wakuu wote wa dunia hii ni lazima wamwangukie yeye, maana ndiye mwenye hatma ya kila mwanadamu. Kumbe ili tuwe na mwisho mwema, yatupasa kumwamini na kumfuata Yesu, maana ndiye Kuhani mkuu aliyetupatanisha na Mungu.

Uwe na wiki njema yenye Utukufu wa Mungu.