Date: 
21-06-2022
Reading: 
Yuda 1:1-4

Jumanne asubuhi tarehe 21.06.2022

Yuda 1:1-4

1 Yuda, mtumwa wa Yesu Kristo, ndugu yake Yakobo, kwa hao walioitwa, waliopendwa katika Mungu Baba, na kuhifadhiwa kwa ajili ya Yesu Kristo.

2 Mwongezewe rehema na amani na upendano.

3 Wapenzi, nilipokuwa nikifanya bidii sana kuwaandikia habari ya wokovu ambao ni wetu sisi sote, naliona imenilazimu kuwaandikia, ili niwaonye kwamba mwishindanie imani waliyokabidhiwa watakatifu mara moja tu.

4 Kwa maana kuna watu waliojiingiza kwa siri, watu walioandikiwa tangu zamani hukumu hii, makafiri, wabadilio neema ya Mungu wetu kuwa ufisadi, nao humkana yeye aliye peke yake Mola, na Bwana wetu Yesu Kristo.

Msigombane njiani;

Waraka wa Yuda hutoa mifano ya watu walioadhibiwa na Mungu kwa sababu ya uovu. Kwa sehemu, katika somo la leo asubuhi, Yuda analiasa Kanisa kuishindania imani kama ilivyohubiriwa kwa wote. Bwana hatasita kuwaangamiza wote wasioamini.

Mungu alituumba ili tukae kwa pamoja tukimwabudu na kumtumikia. Ibada zetu na utume kwa ujumla ni alama ya shukrani na utii kwa Mungu. Ili tuwe na ibada nzuri kwa Mungu, tukae pamoja kwa maana tunaabudu wote.

Tusigombane njiani.