Date: 
13-06-2022
Reading: 
Yohana 3:33-36

Jumatatu asubuhi tarehe 13.06.2022

Yohana 3:33-36

33 Yeye aliyeukubali ushuhuda wake ametia muhuri ya kwamba Mungu ni kweli.
 
34 Kwa kuwa yeye aliyetumwa na Mungu huyanena maneno ya Mungu; kwa sababu hamtoi Roho kwa kipimo.
 
35 Baba ampenda Mwana, naye amempa vyote mkononi mwake.
 
36 Amwaminiye Mwana yuna uzima wa milele; asiyemwamini Mwana hataona uzima, bali ghadhabu ya Mungu inamkalia.

Mungu mmoja;

Baba, Mwana na Roho Mtakatifu;

Yesu anaelezea Mungu wetu alivyo, kwamba amkubaliye Baba, humkubali Mwana na Roho Mtakatifu. Anaonesha kuwa ni Mungu mmoja, maana asiyemwamini Baba hamwamini Mwana wala Roho Mtakatifu na wala hawezi kuurithi uzima wa milele.

Mungu wetu ni mmoja atendaye kazi katika nafsi tatu. Hawa siyo miungu watatu, na wala hakuna aliye juu ya mwingine. Tuliumbwa kwa mfano wa Mungu, tukaokolewa na Yesu kwa njia ya kifo msalabani aliyetupatanisha na Baba, na Roho Mtakatifu hututakasa Roho zetu. Huyu ndiye Mungu tunayemwamini.

Je, wamwamini katika kweli?

Uwe na wiki njema.