Date: 
06-04-2022
Reading: 
Yohana 12:44-20

Hii ni Kwaresma 

Jumatano asubuhi tarehe 06.04.2022

Yohana 12:44-50

44 Naye Yesu akapaza sauti, akasema, Yeye aniaminiye mimi, haniamini mimi bali yeye aliyenipeleka.

45 Naye anitazamaye mimi amtazama yeye aliyenipeleka.

46 Mimi nimekuja ili niwe nuru ya ulimwengu, ili kila mtu aniaminiye mimi asikae gizani.

47 Na mtu akiyasikia maneno yangu, asiyashike, mimi simhukumu; maana sikuja ili niuhukumu ulimwengu, ila niuokoe ulimwengu.

48 Yeye anikataaye mimi, asiyeyakubali maneno yangu, anaye amhukumuye; neno hilo nililolinena ndilo litakalomhukumu siku ya mwisho.

49 Kwa sababu mimi sikunena kwa nafsi yangu tu; bali Baba aliyenipeleka, yeye mwenyewe ameniagiza nitakayonena na nitakayosema.

50 Nami najua ya kuwa agizo lake ni uzima wa milele; basi hayo ninenayo mimi, kama Baba alivyoniambia, ndivyo ninenavyo.

Yesu Kuhani mkuu;

Yesu anaonesha kuwa yeye amwaminiye yeye humwamini yeye aliyempeleka, yaani Baba aliye mbinguni. Yeye amtazamaye amtazama Baba. Yesu anazidi kueleza kuwa yeye amkataaye amkataa Baba wa mbinguni! Kwa sababu Yesu Kristo mwenyewe hufanya kama alivyoagizwa na Baba.

Yesu hapa anatuonesha jinsi alivyo mpatanishi kati yetu na Mungu. Ni kupitia yeye tumeokolewa. Yeye ndiye Kuhani aliyetuokoa mbele za Mungu wetu. Tukimwamini yeye tunamwamini Mungu wa kweli, maana tukimkataa yeye twamkataa Mungu wa kweli.

Siku njema.