Date: 
08-04-2022
Reading: 
Yeremia 46:27-28

Hii ni Kwaresma 

Ijumaa asubuhi tarehe 08.04.2022

Yeremia 46:27-28

27 Lakini usiogope wewe, Ee Yakobo, mtumishi wangu; wala usifadhaike, Ee Israeli; kwa maana, tazama, nitakuokoa toka mbali, na wazao wako toka nchi ya uhamisho wao; na Yakobo atarudi, naye atatulia na kustarehe, wala hapana mtu atakayemtia hofu.

28 Usiogope wewe, Ee Yakobo, mtumishi wangu, asema Bwana; kwa maana mimi ni pamoja nawe; maana nitawakomesha kabisa mataifa yote huko nilikokufukuza, bali sitakukomesha wewe kabisa; lakini nitakurudi kwa hukumu, wala sitakuacha bila adhabu.

Yesu Kuhani mkuu;

Bwana alimtuma nabii Yeremia kupeleka ujumbe kwa taifa la Israeli kuwa asingewatupa, angewaokoa na uzao wao. Yeremia anawatia moyo Israeli kutoogopa, maana Mungu anatangaza kuwaepusha na mabaya yote.

Ujumbe huu asubuhi hii unatukumbusha ahadi ya Mungu kwetu, ya kuwa nasi hadi ukamilifu wa dahari. Yesu aliahidi kuwa nasi siku zote, hivyo tukimtegemea hutuepusha na mabaya yote. Huu ndiyo upatanisho udumuo kati ya Mungu na sisi. Mshike Yesu aliyeahidi kuwa nasi, ili uwe na mwisho mwema.

Siku njema.