Event Date: 
07-04-2021

Akitoa neno la siku ya Ijumaa Kuu, Msaidizi wa Askofu wa KKKT Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Dean Chediel Lwiza aliwaasa washarika kuitumia siku hiyo kutafakari matendo yao na kumrudia Mungu. “Ijumaa Kuu kama tunavyoiita sisi wakristo ni siku ya huzuni sana kwetu kwani Yesu tunayemtaja kila siku alikufa msalabani kwa ajili ya dhambi zetu. Hivyo sisi wakristo wa leo tuna deni kubwa kwake. Ijumaa Kuu sio tu siku ya kumbukumbu, inabidi ibadilishe kitu katika maisha yetu ya kila siku,” alisema Dean Lwiza. Katika hatua nyingine, Dean Lwiza aliongoza maombi maalum kwa ajili ya taifa la Tanzania, Kanisa pamoja na kwa ajili ya washarika wote waliohudhuria ibada hiyo ambayo iliambatana na igizo la mateso ya Yesu Kristo lililochezwa na vijana wa usharika.

Angalia picha  nyingine hapa https://drive.google.com/drive/folders/1oJUu_Z3hQE1rXj_Yb040roCLGM458OCa...