Date: 
01-11-2021
Reading: 
Yakobo 1:22-25

Jumatatu asubuhi 01.11.2021

Yakobo 1:22-25

[22] Lakini iweni watendaji wa neno, wala si wasikiaji tu, hali mkijidanganya nafsi zenu.
 
[23] Kwa sababu mtu akiwa ni msikiaji wa neno tu, wala si mtendaji, mtu huyo ni kama mtu anayejiangalia uso wake katika kioo.
 
[24] Maana hujiangalia, kisha huenda zake, mara akasahau jinsi alivyo.
 
[25] Lakini aliyeitazama sheria kamilifu iliyo ya uhuru, na kukaa humo, asiwe msikiaji msahaulifu, bali mtendaji wa kazi, huyo atakuwa heri katika kutenda kwake.

 

Mwenye haki ataishi kwa imani;

Leo asubuhi tunasoma juu ya kusikia neno la Mungu na kuwa watendaji. Yaani kusikia neno la Mungu na kulifanyia kazi. Kulisikia neno likatuongoza ni mwanzo wa kuwa na heri duniani.

Hakuna kuishi kwa Imani bila neno la Mungu, maana ndiyo msingi wenyewe. Neno hutafanya kuwa imara, hivyo kuwa watu wenye ushuhuda. Hivyo tuwe wenye kusoma, kusikia, na kuwa watendaji wa neno, ili tuweze kuwa wenye haki mbele za Mungu, tukimshuhudia bila kukoma.

Nakutakia wiki njema yenye ushuhuda na mafanikio.